UONGOZI HANDENI WAKUTANA NA WANANCHI KUWAPA ELIMU YA KUACHA KUVAMIA MAENEO YA WAWEKEZAJI WALIOMILIKISHWA KISHERIA


Wawekezaji wa AMC Ltd na viongozi kutoka halmashauri wakisoma ramani ya eneo la shamba la mkonge la kwamgwe.
Mkurugenzi mtendaji  Bw. William  Makufwe  akizungumza na wananchi wa vijiji vya bondo na majanini kata ya kwamgwe.
Mkuu wa wilaya ya halmashauri ya wilaya ya handeni Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya bondo na majanini  kata ya kwamgwe
Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya handeni  Bw. Mangesho akiwaeleza wananchi kuwa kukaa muda mrefu sehemu haimaniishi ndio mtu anakua navumiliki halali wa eneo.
Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wakijitambulisha kwa wananchi wa vijiji vya bondo na majan
Mh. Sharifa Abebe diwani wa kata ya kwamgwe  akishukuru uongozi wa halmadhauri, wawekezaji na wananchi kwa kufikia muafaka.
Baadhi ya wananchi wa vijiji vya bondo na majanini  na walioketi viti vya mbele ndio viongozi wa kampuni ya AMC ltd.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri pamoja na wawekezaji wa shamba la mkonge la Kwamgwe Kampuni ya AMC LTD wamefanya ziara na kuongea na wananchi wa Vjiji vya Bondo na Majanini namna ya kuachia maeneo ambayo wananchi hao wamevamia katika shamba hilo kwa kufanya makazi na kulima mazao ya kudumu hali iliyopelekea muwekezaji huyo kushindwa kuendelea na shughuli zake.

Akizungumza na wananchi mwakilishi wa Mkurugenzi bodi ya mkonge Bw.Fredrick Sospeter alisema shamba hilo ni mali ya kampuni ya AMC LTD ambayo walinunua toka 2002 baaada ya CRDB BANK kutangaza kuuza eneo hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa mwekezaji wa awali aliyejulikana kwa jina la CHAVDA kushindwa kurejesha fedha za mkopo alizokuwa akidaiwa na hivyo kuamua kuliuza shamba hilo ili kufidia deni alilokua akidaiwa.

BW. Fredrick alisema kuwa awali serikali ilipanga kutoa ekari 500 kwa wanachi waliovamia ili wapate eneo la kulima na kuacha eneo la mwekezaji wazi ili kuruhusu shughuli za mwekezaji kuendelea. Dhamana hiyo imechukuliwa na mwekezaji AMC kugawa ekari 500 ambapo ekari 200 zitagawiwa kwa wananchi wa kijiji cha Bondo na ekari 300kijiji cha majanini. Ilielezwa kuwa watakao gaiwa watakuwa ni wale waliovamia na kukaa kwa muda mrefu. Mgao huo utakua pembezoni mwa Kijiji ambapo kimeishia na kwamba maeneo ya kulima yatakua ndani ya Kijiji husika.


Wananchi wanaolima mazao ya kudumu utaratibu utawekwa ili kuwawezesha wananchi hao kuvuna mazao yao na hatimaye kutoa mazao yao shambani humo, aidha wananchi ambao wanadai viinua mgongo vyao serikali inapanga utaratibu wa namna ya kuwalipa.

Mkuu wa wilaya Mh. Godwin Gondwe aliwaeleza wananchi kuwa watu watakaopewa ardhi hiyo wanafahamika kwani orodha yao ilikwisha andaliwasiku za nyuma. Pia aliwawaondoa wasiwasi wananchi kwamba shule, nyumba za ibada na zahanati ambazo tayari wamezijenga zitaendelea kutumika bila kuharibiwa kwa namna yoyote ile. 

Wananchi ambao wanaishi kwenye nyumba za mkonge wataendelea kuishi pia ila wasijenge nyingine, aliwaonya viongozi au mwanachi yeyote ambaye atathubutu kuuza eneo ambalo mwekezaji atalitoa kwaajili ya kilimo kwa wakazi wa vijiji hivyo atachukuliwa hatua za kisheria maramoja kwani serikali ya awamu ya tano inasimamia sheria na haki kwa kila mtu na hivyo wasiwe na wazo la kuuza eneo lolote.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. William Makufwe aliwaeleza wananchi kwamba wamekuja kutoa ufafanuzi wa kisheria juu ya umiliki halali wa shamba hilo. Aliwaeleza kuwa wawekezaji wanakuja kufanya maendeleo katika maeneo yetu hivyo tuwape muda wafanye kazi. Aidha aliwataka wawekezaji hao kupeleka mpango kazi wa shamba hilo ili waweze kujua kama eneo wanaweza kuliendeleza au hawawezi ili hatua stahiki za kisheria ziweze kutekelezwa ikiwa kampuni itashindwa kuliendeleza shamba hilo kwa mujibu wa makubaliano.

Diwani wa Kata ya Kwamgwe Mhe. Sharifa Abebe aliwashukuru viongozi na wawekezaji, nakuwaomba waainishiwe hizo ekari ili waanze kufanya kazi maramoja,wameomba wawekezaji watakavyoanza kufanya kazi kipaumbele katika ajira kiwekwe kwa wakazi wa maeneo hayo. 

Uongozi wa kampuni ya AMC LTD uliwataka waliolima mazao ya michungwa na mazao mengine ya kudumu kuandika barua hadi kufikia tarehe 25/10/2016 kwa mwekezaji wakitaja majina yao, mazao wanayolima, wanaomba mazao yao yakae kwa kipindi gani hadi watakapoyavuna yote. Watendaji wametakiwa kukaa ofisini kuanzia saa moja na nusu hadi saa tisa na nusu kuwasaidia wananchi namna ya kuandaa barua hizo.


Alda P Sadango
Afisa habari 
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
18 Octoba 2016.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA