Video: Mpambano Wa Isha Mashauzi, Malkia Leyla Ulikuwa ‘Balaa’!


dar-live1

MASHABIKI wa burudani,  hususan muziki wa taarab, usiku wa kuamkia jana walipata burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki huo, Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla Rashid kwa upande mwingine akiwa na kundi  lake la Jahazi Modern Taarab, walipotoana kijasho  kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani mkali kati yao.
Kabla ya mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande fulani ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema “aaah, wapi bwana Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa nini”!
Hatma ya ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha mashabiki wakijionea na kuamua wenyewe. Kabla ya wakali hao kupanda jukwaani mshereheshaji wa shughuli hiyo,  Aisha Mbegu, wa Redio Times ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kulivamia jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha ndiye aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.
(PICHA/HABARI:  RICHARD BUKOS /GPL)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.