VYUO VYA HABARI VIJIANDAE KUTOA ELIMU BORA ILI KUENDANA NA MABADILIKO YATAKAYOLETWA NA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI.


Mapema Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari nchini.

Kwa sasa Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa na wabinge.

Sasa hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwa katika kanuni.

Ukisoma kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.

Tukiangali kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya mitihani ya kufuzu ili kudhitishwa.

Kwa waandishi wa Habari pia tutegemee kuwepo kwa vigezo na masharti ambayo kwa vitahitaji kuongeza elimu tulizonazo katia fani yetu na pia hili litasababisha sasa vyuo vya uandishi wa habari na mawasiliano kutoa elimu iliyo bora zaidi ili kuendana na mabadiliko haya.

Tumeshudia uwepo wa vyuo vya uandishi wa habari kila sehemu hata vingine ukiangalia mazingira yake lazima utilie shaka kama vinatoa ile elimu inayostahili na iliyodhibitishwa na mamlaka zilizopo za TCU na NACTE. 

Niwaombe tu wahusika katika vyuo vya uandishi wa habari kuzingatia vigezo na masharti ya utoaji wa elimu ya Habari na Mawasiliano katika vyuo vyao kwani kuja kwa Sheria ya Huduma za Habari ni mwanzo wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taalum inayoheshima na kuwa taaluma inayoheshimika sana na sio rahisi kuipata kama sasa watu wanavofikiria tu ukitaka kuwa mwandishi wa habari unaweza kusoma miezi mitatu hivi basi umekuwa mwandishi wa habari.

Ingawa kuna baadhi watu wanasema wanatumia vipaji vyao vya uandishi wa habari na utangazaji lakini tujue kuwa kipaji bila ya kuendelezwa ni kazi bure tunahitaji kuviendeleza vipaji hivyo kwa kupata elimu na ujuzi zaidi wa fani ya habari ili kuendana na mabadiliko ya teknlolojia na Sheria za nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*