WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA ONYO KWA MAJANGILI

Ofisa Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Twaha Twaibu akitoa mada ya hali ya ujangili nchini na changamoto
mbalimbali za kukabiliana na ujangili katika kongamano la kupiga vita ujangili jijini Arusha jana. (NA MPIGAPICHA WETU)

Wizara ya maliasili na utalii imetoa onyo kwa majangili wote nchini wanaojihusisha na vitendo haramu vya ujangili wa wanyamapori kuwa siku zao zinaesabika baaada ya kuunda kikosi cha Wizara cha kukabiliana na ujangili
ambacho kinahusisha na vyombo vingine vya usalama. 

Hayo yalisemwa jana na Bw, Twaha Twaibu ambaye ni Afisa wanyamapori Mkuu na vilevile ni afisa habari na mawasiliano kutoka wizar aya maliasili na utalii, akifuatana na Waziri wa Wizara Prof. Maghembe katika Kongamano hilo la kupiga vita
ujangili, Bw. twaha alitoa mada ya hali ya ujangili nchini na changamoto mbalimbali za kukabiliana na ujangili na kuwaelezea wajumbe mkakakti ambao wizara imejiwekea katika kupambana na ujangili.

Alitoa wito kwa wananchi wote wanajihusisha naujangili kuancha mara moja vinginevyo wataingia kwenye mikono ya dola na kutelekeza familia zao.

Mada hiyo ya Bw, Twaha aliwasisismua wajumbe kutoka Tanzania Bara na visiwani ambayo walikuwa makini sana kumsikiliza Bw. Twaha maswali mbalimbali ya kuhusu ujangili aliyajibu kwa ufasaha akisaidiwa na Mkurugenzi toka TANAPA Dr, Dembe ambaye ndiye alifunga Kongamanop hilo baada ya kufunguliwa na waziri wa maliasili na utalii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU