YANGA YAFUKUZA BENCHI LOTE, YALETA MZAMBIA NA KUMREJESHA MKWASA


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BENCHI lote la Ufundi la Yanga SC litaondoka na watakuja watu kabisa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi na Wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo wataondoka.
Na Mzambia, George Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.  
Kocha Mzambia, George Lwandamina anatakiwa kuchukua nafasi ya Pluij Yanga 

Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE imezipata kutoka ndani ya Yanga zimesema kwamba klabu inaendelea na mazungumzo na Lwandamina.
“Mazungumzo yanaendelea, tutakapokubaliana atakuja kusaini,”kimesema chanzo.
Na kuhusu watendaji wapya wa benchi la Ufundi wazalendo, chanzo kimesema; “Hao wote wamependekezwa na kwa kuwa ni watu wetu, ni suala la kuzungumza nao tu,”.
Pluijm amejikuta katika wakati mgumu baada ya Yanga kuambulia pointi 11 kati ya 18 za mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC imetoa sare mbili, imefungwa mechi moja na kushinda tatu tangu kuanza kwa Ligi Kuu – hiyo ikiwa ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Azam kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2.
Na baada ya mchezo wa Oktoba 1, wakilazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu, Simba SC waliokuwa pungufu kwa sehemu kubwa kufuatia Nahodha wao, Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29, baadhi ya viongozi wa Yanga wamependekeza mwalimu huyo aondolewe

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)

WAGGGS AFRIKA WAIPONGEZA TGGA KWA KUONGOZA AFRIKA KUSAJILI GIRL GUIDES WENGI