AVEVA AITISHA KAMATI YA UTENDAJI SIMBA LEO


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Simba SC inakutana leo katika kikao cha dharula mjini Dar es Salaam kupitia taarifa ya benchi la Ufundi baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva alisema kwamba amewatumia taarifa Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya Simba kuwaita kikao cha kesho kujadili mustakabali wa klabu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Evans Aveva ameitisha kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC leo mjini Dar es Salaam

Ajenda kuu katika kikao cha leo ni taarifa ya benchi ya Ufundi chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog, lakini pia taarifa nyingine mbalimbali zitajadiliwa.
Lakini Aveva alisema; “Kikubwa ni tutakuwa na kikao, suala ajenda hiyo ni siri yetu,”.
Moja ya mambo yanayotarajiwa kwenye ripoti ya benchi la Ufundi ni mapendekezo ya wachezaji wa kusajiliwa kuiongezea timu nguvu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.  
Simba SC ilifanikiwa kumaliza Ligi Kuu kileleni kwa kujikusanyia pointi 35, mbili zaidi dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC.
Na moja ya mikakati ya awali ya maandalizi ya Simba SC kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ni timu kwenda Ethiopia kwa michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu. 
Kwa sasa wachezaji wa timu hiyo wapo mapumzikoni hadi mapema Desemba watakapokutana tena kwa maandalizi ya mzunguko wa pili, ambayo yatahusisha pia na safari ya Ethiopia.  
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI