FILAMU NA TAMTHILIA ZA KITANZANIA ZAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM ZITARUSHWA NA DSTV



Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu na Tamthilia za Kitanzania zitakazorushwa na DSTV kupitia Chaneli yao kuanzia Maisha Magic Bongo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi.
Wadau wa filamu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.
Wasanii wa filamu na wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Taswira katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) na viongozi wengine wakizindua Filamu na Tamthilia za Kitanzania.
Na Dotto Mwaibale
TANZANIA imeingia katika mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu baada ya Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na Multchoice Tanzania pamoja na maprodyusa kuzindua rasmi chaneli yao (160) Maisha Magic Bongo itakayo kuwa ilirusha filamu na tamthilia za kitanzania.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu na Tamthilia za kitanzania kwa niaba ya Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alisema mpango wa kurusha filamu za kitanzania kupitia mtandao wa DSTV utasaidia sana kutangaza filamu zetu na kuleta ushindani katika ulimwengu wa kimataifa.
“Serikali tunaona hili ni jambo muhimu sana litakalowafanya wadau wa kazi za kitanzania kutabasamu tena kwani sote tunafahamu umaarufu wa chaneli zilizopo DSTV na jinsi zinavyoweza kuwafikia watu wengi duniani” alisema Fissoo.
Aliongeza kuwa uzinduzi huo uliohusisha filamu sita, tamthilia mbili na kazi nyingine mbili DSTV wametoa mtaji wa dola za kimarekani 450,000.
Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi alisema uzinduzi huo umelenga kusherehekea kazi nzito za maprodyusa wa filamu hapa nchini na utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye maudhui ya kitanzania.
Alisema chaneli hiyo imelenga kuburudisha na kuelimisha watamazaji wa kitanzania kupitia filamu, tamthilia na maigizo mbalimbali ya kiswahili.
Aliongeza kuwa chaneli hiyo itapatikana kwenye kifurushi cha huduma za DSTV (160).

Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.
Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage alisema mpango huo utasaidia kukuza lugha ya kiswahili kama alivyokuwa akifanya mtunzi wa mashairi hayati marehemu Shabani Robert katika kukuza lugha hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA