JAFO AWAONYA WAFANYABISHARA WANAOPANGA BIDHAA BARABARA ZA DODOMA


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa ya Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akipokea maelezo ya ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa ya Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa ya Dodoma.
 Dampo la kisasa lilojengwa katika eneo la Chidaye Manispaa ya Dodoma.
 :Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi la Dampo la kisasa lililopo eneo la Chidaye nje kidogo ya manispaa ya Dodoma.
   Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi kuhusu ujenzi wa  Dampo la kisasa eneo la Chidaye.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi kuhusu mtaro uliopo katika Dampo la kisasa eneo la Chidaye.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika manispaa ya Dodoma huku akipiga marufuku wafanyabiashara kupanga bidhaa zao kwenye barabara na kuwataka wafanye biashara zao kwenye masoko au maeneo rasmi yaliyotengwa na Manispaa hiyo.

Akizungumza leo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Sango iliyopo katika soko kuu la majengo na ujenzi wa dampo la kisasa,Jafo amesema serikali inawekeza fedha nyingi kwenye barabara lakini mwisho wa siku barabara haionekani kutokana na watu kupanga bidhaa zao.

Naibu Waziri huyo amesema kupangwa kwa bidhaa za nyanya au vitunguu barabarani kumekuwa kukichafua barabara na wakati mwingine kusababisha zisipitike kiurahisi na watumiaji wengine.

Ameagiza Manispaa hiyo kuhakikisha malengo ya barabara hiyo yanafuatwa na kuwazuia wafanyabiashara hao ili barabara hizo zitunzwe ziweze kudumu na kufikia malengo.

“Hivi karibuni nilitembelea barabara hii na ilikuwa ni mbaya na ni eneo la kibiashara niliagiza Manispaa kuhakikisha barabara hii inajengwa, nimefarijika sasa agizo limetekelezwa,”amesema Jafo

Hata hivyo amesema kwa kuwa vikao vimeanza vya kupendekeza Dodoma iwe jiji ni lazima ibaki maana yake na thamani ya jiji ipatikane kwa  watu kuweka bidhaa zao kwenye masoko yanayotakiwa.

Kuhusu Dampo la kisasa lililopo eneo la Chidaye mjini Dodoma,  Jafo ameitaka manispaa kuhakikisha eneo hilo halivamiwi na watu kwa kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kuvamia maeneo yanayojengwa miundombinu.

Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi amemuahidi Jafo kuwa atasimamia sheria ndogo ndogo za manispaa kuhakikisha wafanyabishara wanafanya biashara zao kwenye maeneo yaliyopangwa.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI