Maafisa wa TPA na TRA waanza Mafunzo mara baada ya TPA kukamilisha ufungaji wa ‘Scanner’ mpya Bandari ya Dar es Salaam


 
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akifungua mafunzo hayo kwa Watumishi wa TPA na TRA yanayohusu matumizi ya ‘scanner’ mpya iliyofungwa katika Bandari ya Dar es Salaam.

 Baadhi ya Watumishi wa TPA ambao watahusika na usimamizi wa matumizi ya ‘scanner’ mpya wakati wa ukaguzi wa mizigo ya kontena katika Bandari ya Dar es Salaam.

 Afisa Forodha Mwandamizi wa TRA, Bw. Julius Joseph akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo alitoa rai kwa TPA na TRA kuendelea kushirikiana kwa pamoja wakati wa ukaguzi wa mizigo katika Bandari za Tanzania ili kuondoa mianya ya ukwepaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali.

 Afisa Ufundi anayehusika na scanner kutoka TRA, Bw. Manjale Musele akichangia jambo kuhusiana na namna walivyojipanga katika kuhakikisha ‘scanner’ mpya inatumika kikamilifu ili kuisaidia Serikali kuongeza mapato.

 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ambapo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wakati watakapokuwa wanaendesha scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Fredy Liundi, Kaimu Mkurugenzi wa Utumishi, Bw. Erasmo Mbilinyi na Kaimu Mkurugenzi wa Tehama, Bw. Abdulrahman Mbamba (kulia).

 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deudedit Kakoko akifurahia jambo na Meneja Mafunzo kutoka Kampuni ya Nuctech ya Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Lan Yuming mara baada ya kuzindua mafunzo kwa Maafisa wa TPA na TRA hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Nuctech Bw. Zhang Sheng.
Jengo jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya matumizi ya scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR