MADEREVA 62 WA UDART WACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU


ukal
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Suleiman Jafo akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge wakati wa kikao cha sita cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 8, 2016.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.
Jumla ya madereva 62 wanaoendesha mabasi yaendayo haraka (UDART) wamechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu ya kukiuka Sheria za barabarani.
Idadi hiyo ya madereva imetajwa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe Suleimani Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Mohammed lililohoji kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya madereva hao ambao hawafuati sheria za barabarani.
Mhe. Jafo amekiri kuwa madereva hao wamekuwa wakiendesha mabasi hayo kwa kasi kubwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya watu waendao kwa miguu lakini madereva hao wanapaswa kuzingatia Sheria za usalama barabarani kama ilivyo kwa madereva wanaoendesha aina nyingine ya magari.
“Tangu mabasi haya yaanze kutoa huduma, tumeshawachukulia hatua za kinidhamu madereva 62 ambapo kati ya hao, madereva 20 wamepewa onyo kwa makosa ya usalama barabarani, wawili wamefukuzwa kazi na madereva 40 wamekatwa mishahara yao kwa makosa mbalimbali ya barabarani”, alisema Mhe. Jafo.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa mabasi hayo yamefungwa vifaa maalum kwa ajili ya kutoa ishara ya dereva anayezidisha mwendo wa zaidi ya Kilomita 50 kwa saa moja ili kudhibiti mwendo mbaya wa mabasi hayo.
Aidha, ili kuwakumbusha taratibu na maadili ya kazi ya udereva Mhe. Jafo ameeleza kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kuwajengea uwezo madereva hao kupitia semina zinazoendeshwa na wataalam kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) pamoja na Askari wa Usalama Barabarani.
Amefafanua kuwa watoa huduma wanatakiwa kuzingatia muda katika kutoa huduma mkataba baina ya DART na mtoa huduma ambaye ni U- DART unaoainisha kuwa huduma ya mabasi yaendayo haraka itaanza kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi sa 06:00 usiku
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI