MWIJAGE:WANAODAI FIDIA ZAO ENEO LA UWEKEZAJI(EPZ)BAGAMOYO WAVUTE SUBIRA


WAZIRI wa viwanda,biashara na uwekezaji,Charles Mwijage,akizungumza na wafanyakazi wa  kiwanda cha Eiven industry cha kuchakata matunda na kukausha matunda kilichopo wilayani Bagamoyo.

WAZIRI wa viwanda,biashara na uwekezaji,Charles Mwijage,akizungumza na wafanyakazi wa  kiwanda cha Eiven industry cha kuchakata matunda na kukausha matunda kilichopo wilayani Bagamoyo.

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZIRI wa viwanda,biashara na uwekezaji,Charles Mwijage,amewataka baadhi ya wananchi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wanaotakiwa kulipwa fidia ili kupisha mradi wa eneo la uwekezaji EPZ na bandari,wavute subira ,kwani serikali iko mbioni kukamilisha malipo hayo.
Amesema hakuna kitu kinachomnyima usingizi kwasasa kama fidia ya watu hao kutokana na kwamba walishaambiwa wasiendeleze maeneo yao kwa ajili ya mradi huo.
Aidha ameahidi kumpatia eneo lenye hekari 50 bure,mmiliki wa kiwanda cha Eiven industry cha kuchakata matunda na kukausha matunda kilichopo wilayani Bagamoyo ,alizoomba ili kujenga kiwanda kingine .
Katika hatua nyingine Mwijage,amewataka wananchi ,kutunza maeneo yao na kulima kisasa hasa mazao ya matunda ili kuzalisha kwa wingi malighafi hiyo na kupata soko la uhakika.
Hayo aliyasema mkoani Pwani,wakati wa ziara yake ya siku moja yenye lengo la uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda katika mkoani hapo,jijini Dar es salaam na Tanga.
Mwijage alisema wapo baadhi ya wananchi ambao wameshalipwa kupisha eneo la uwekezaji EPZ Bagamoyo na wengine bado hivyo wizara yake inaendelea kulisimamia suala hilo.
“Kitu kizuri hakihitaji haraka ,na kizuri shurti kiwe na uchungu,ninachowaomba wavute subira kwani mradi huu ni mkubwa na wenye tija kiwilaya ,mkoa na taifa kijumla”alisema Mwijage.
Hata hivyo Mwijage licha ya kuwataka wananchi kutunza maeneo na kulima kisasa,pia aliwaasa kusomesha watoto wao.
Alieleza kwamba watoto wasome wasisubiri wakuja waje nchini ndio waje kufanyakazi wakati wazawa wapo.
Mwijage alisema miongoni mwa kero zilizopo nchini ni ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo nguzo kuu ni kusomesha watoto hususan kwenye ujasiriamali.
Waziri Mwijage aliupongeza mkoa wa Pwani chini ya juhudi za mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo kwa kuwa mbele kwa kasi ya kujenga viwanda ambavyo vitasaidia na kuwezesha kutoa ajira na kukuza uchumi.
Katika ziara hiyo, alitembelea kiwanda cha dawa za viuadudu vienezavyo malaria (Biotec products)kilichopo Kibaha ,global packing kinachotengeneza mascania kilichopo Tamco Kibaha.
Viwanda vingine ni Eiven industry cha kuchakata na kukausha matunda kwa ajili ya kuuza nje ya nchi na ndani kilichopo Chalinze,kiwanda cha sayona kinachosindika mananasi na nyanya kilichopo Bagamoyo.
Msimamizi wa kiwanda cha Eiven alisema endapo akipatiwa eneo lenye hekari 50 atajenga kiwanda kingine na kuanza kuzalisha baada ya mwaka mmoja .

Akiwa katika kiwanda cha Biotec products alisema ni kiwanda pekee ambapo ameridhika nacho na kuongeza kuwa kinakwenda vizuri.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,alishukuru kwa ujio wa waziri huyo mkoani humo.
Alisema amedhamiria mkoa huo kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji ambapo hadi sasa umetenga maeneo yenye hekta 19,600 na hekari 3,266 kwa ajili ya uwekezaji.
Mhandisi Ndikilo,alifafanua kwamba tayari kuna viwanda 88 ambavyo ni vikubwa ,vya kati na vidogo huku miradi 10 ya kimkakati ipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.
Alisema atavalia njuga suala la uwekezaji ili kuhakikisha mkoa unapiga hatua kiuchumi baada ya miaka mitano.

Awali mwenyekiti wa CCM Bagamoyo,Maskuzi alisema mradi wa EPZ katika eneo la kujenga bandari  ni mkubwa lakini wananchi bado wapo kwenye sintofahamu ya fidia zao .

Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.