NSSF YASHIRIKI KONGAMANO LA VIWANDA CHUO KIKUU UDSM


Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeshiriki katika kongamano la kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda, kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akiongea kwa niaba ya wadhamini wa kongamano hilo, Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, alisema NSSF kama sehemu ya jamii inao wajibu wa kushiriki katika uendelezaji wa viwanda kwa kuwa uelekeo huo utazalisha ajira nyingi ambapo waajiriwa hao watakuwa wanachama wa mfuko wa NSSF na itapata michango na kuiwekeza na baadae kuilipa kama Pensheni pindi ajira zao zitakapokoma.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akitoa mada wakati wa kongamano la siku mbili la wanataaluma kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda na mageuzi ya jamii. Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Nkurumah jijini Dar es Salaam jana na kudhaminiwa na NSSF. Kushoto ni Prof. Sam Maghimbi. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara na Prof. Sam Maghimbi (kushoto), wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko na Uhusino, Anna Nguzo (kulia), kuhusu mwamko wa wanachuo kujiunga na NSSF baada ya kupata elimu ya mafao yanayotolewayo na NSSf. Wanachuo wanaweza kujiunga na NSSF kupitia Scheme ya AA PLUS (Afya na Akiba kwa Wanachuo).  Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kujiunga na NSSF wakati wa kongamano la siku mbili la wanataaluma kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda na mageuzi ya Jamii. Kongamano hilo limedhamiwa na NSSF.
Wanachuo na wadau wakiwa katika kongamano hilo.
Wanachuo na wadau wakiwa katika kongamano.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro akitoa mada kuhusu mafao yatolewayo na NSSF.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro akitoa maelezo kwa wanachuo wa UDSM, kabla ya kujiunga na NSSF wakati wa kongamano la siku mbili la wanataaluma kuhusu ujenzi wa uchumi wa viwanda na mageuzi na Jamii. Kongamano hilo limedhamiwa na NSSF.
Wanachuo wakipata maelekezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF.
Ofisa Masoka na Uhusiano NSSF, Anna Nguzo akiwaelimisha wanachuo mafao yatolewayo na mfuko wa NSSF.
Wanachuo wakijiandikisha.
Ofisa Mwandamizi Sekta Binafsi wa NSSF, Abbas Cothema atoa maelekezo kwa mmoja wa wanachuo wa UDSM wakati akijaza fomu ya kujiunga na NSSF.
 Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amina Mmbaga (kulia), akiwaelimisha wanachuo jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na NSSF.
 Afisa wa NSSF akiwaandikisha wanachuo.
  Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amina Mmbaga (kushoto), akiwaelimisha wanachuo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU