PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI

 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja ya picha ya ndege  22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.Kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange.
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (katikati) akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu  maandalizi wa mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitakazotua nchini Novemba 28 na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange na Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.
 Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari
 Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya Ndege ya kampuni hiyo, Andrew Lauwo (kulia)  akifafanua jambo katika mkutano huo
Mkutano ulivyokuwa


Puma Energy Tanzania Ltd
Kampuni ya puma kuwa mwenyeji wa mashindano ya ndege za zamani
23rd November 2016
Taarifa Kwa umma
Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo ni sehemu ya Puma Group, Kampuni ya kimataifa inayojishughulisha usafishaji mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta yaliyosafishwa tayari kwa matumizi, inayofuraha kujulisha umma kuwa itakua mfadhili mahsusi  katika  mashindano ya anga yanayohusisha ndege za zamani kwa mwaka 2016.
Vintage Air Rally inahusiaha ndege za zamani za miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika kuanzia kisiwa cha Crete Ugiriki hadi Cape town Afrika ya kusini.
Shindano hili lilianza tarehe 12/11/2016 kule Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35  katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika ya Kusini.
Shindano hili linalengo la kutahini ujuzi wa marubani husika,  na wakati huohuo kuchangisha fedha kwa ajili ya mashirika ya Kimataifa ya hiari UNICEF, Bird life International and Seed Bombing. Sisi kama Puma tunasikia fahari sana kuwa sehemu ya uvumbuzi huu wa ajabu. 
 Kampuni ya Puma Energy inayofuraha kuwa mwenyeji wa mashindano haya.   Ndege zinazotumika katika aina hii ya mashindano huwa zinahitaji aina maalumu ya matengenezo kwa kuzingatia umri wake pamoja na teknolojia iliyotumika. Tumejikita katika kuendela kufanya vyema na pia kuwa na uhakika wa uapatikanaji wa bidhaa ya mafuta na tunafuraha kutoa mchango wetu katika kuhakikisha kwamba mashindano yanayafanyika vyema. Jukumu letu katika kusaidia
kuendeleza utalii ndani ya nchi yetu linabaki kuwa sehemu muhimu sana katika masula yetu ya kijamii kama kampuni katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku, Alisema Philippe Corsaletti, Meneja Mkuu wa Puma Enery Tanzania.
 Vintage Air Rally watatua Tanzania (KIA) tarehe 28/11/2016 wakitokea uwanja wa ndege wa Wilson Nairobi. Marubani watakua na muda mzuri wa kutembelea mbuga zetu za wanyama kama sehemu ya safari yao. Hili pekee pia litasaidia katika kuweka utalii wa nchi yetu katika mtizamo wa kimataifa Zaidi kwani shindano hili linafuatiliwa na maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali duniani.
 Kampuni ya Puma Energy Tanzania imejiandaa kabisa kupokea ugeni huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote za kujaza mafuta ili kuhakikisha urukaji ulio salama. Ndege hizi zinatumia mafuta aina ya Avgas ambayo kwa sasa ni kampuni ya Puma pekee inayotunza hapa nchini. Timu ya watu wetu imejiandaa kupokea na kuhudumia msafara mzima katika kiwanga cha juu cha ubora na ufanisi. Uwepo wa bohari zetu za mafuta ya ndege katika maeneo mbalimbali nchini unafanya iwe rahisi kuhudumia ndege hizo ambao msafara huu utapita.
Kwa hapa Tanzania, Vintage Air Rally Aircrafts zitajaza mafuta Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, Zanzibar, Dodoma, and Songwe kabla ya kuelekea Zambia ambapo watapokelewa na kuhudumiwa na wenzetu wa Puma Zambia.
Tanzania itaweka historia kwa kuwa moja ya nchi chache duniani ambapo mashindano haya yatapita. “Tunawakaribisha wananchi wote katika tukio hili la kihistoria wakati ndege za Vintage zitakapokua zikipita maeneo yenu na kutumia fursa hii kuendeleza utalii”, Alisema Ndugu Philippe.

Kuhusu njia itakayotumika:
Njia inayotumika ni sawa kabisa na ufuatishaji wa safari ya shirika la ndge la Imperial ya mwaka 1931 “safari ya Afrika” ambapo ndege itakua ikiruka chini kupitia Nile kutokea kongo hadi Khartoum, kupitia nyanda za juu za Ethiopia, uwanda wa chini wa Kenya,  na hatimaye sehemu yenye changamko sana ya Afrika Mashariki.  Baada ya hapo itaondoka tena kupitia Kilimanjaro hadi Serengeti, na hatimaye hadi kwenye visiwa vya marashi ya Zanzibar na hadi chini Zaidi, kupitia Zambia, juu ya maporomoko ya Victoria, hadi Bulawayo Zimbabwe. Siku za mwisho za safari hii ndefu inayohitaji pumzi nyingi itawafikisha Botswana na Afrika ya Kusini - Capetown ambapo utakua mwisho wa safari

Kampuni ya Puma Energy ni kampuni ya kimataifa ya viwango vya kati ambayo imejikita katika kusafisha mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta masafi kwa watumiaji katika zaidi ya nchi 45 duniani. Puma Energy iliingia Tanzania mwaka 2012 na hadi sasa inaongoza katika  soko na pia kampuni pekee yenye uwepo katika viwanja vinane hapa Tanzania  ambavyo ni Kilimanjaro, Zanzibar, Songwe, Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, na Julius Nyerere.

Philippe Corsaletti
Meneja Mkuu.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI