SAANYA NA MPENZU SASA KUHOJIWA MBELE YA KAMATI YA SAA 72


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MAREFA Martin Saanya na Samuel Mpenzu wanaotuhumiwa kuvurunda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga Oktoba 1, mwaka huu wameitwa mbele ya Kamati ya Saa 72 ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kuhojiwa.
Taarifa ya Kamati ya Saa 72 leo imesema kwamba wawili hao watahojiwa ili kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika taarifa zao kuhusu mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga walitangulia kwa bao la Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kabla ya mzalendo, Shizza Ramadhani Kichuya kuisawazishia Simba SC iliyocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
Refa Martin Saanya nyuma ya viungo Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) na Muzamil Yassin (kulia) Oktoba 1, mweaka huu Uwanja wa Taifa 

Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya akamtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Na mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani.
Polisi walitumia milipuko kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea na Simba SC wakafanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na winga Shizza Kichuyaa dakika ya 87 baada ya kona aliyochonga kuingia moja kwa moja nyavuni. 
Baadaye Kamati ya Saa 72 ilifuta kadi ya Mkude baada ya kubaini alionyeshwa kimakosa.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA