SERIKALI YATOA MAFUNZO YA TATHMINI NA UFUATILIAJI KUBORESHA UTENDAJI


Serikali imesema itahakikisha inaimarisha uwezo wa kitaasisi ili kumudu vyema kazi za ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo mbalimbali itakayosaidia kuboresha utendaji kazi za Ufuatiliaji na tathmini serikalini. 

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Susan Mlawi alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi. 

Mlawi alisema Mkakati wa Serikali wa kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa taasisi hizo kunatonakana na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa Ufuatiliaji na Tathmini ambao ungetoa suluhisho la changamoto mbalimbali zinazozikabili Taasisi za Umma nchini. 

“Kukosekana kwa mfumo madhubuti wa Ufuatiliaji na Tathmini katika taasisi za umma nchini umesababisha kukwama kwa utekelezaji wa majukumu ya kila siku na utoaji maamuzi sahihi,” 

Bi. Mlawi aliongeza. Alidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Serikali kuwa ni pamoja na baadhi ya taasisi zake kulalamikiwa na wananchi kwa kutoa huduma zisizoridhisha, utendaji ambao haulingani na thamani halisi ya uwekezaji wa fedha za Umma katika taasisi hizo, mchango mdogo wa baadhi ya Taasisi za Umma katika kuchangia mapato katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ongezeko la utegemezi kwa Serikali kuu, uzalishaji na tija ndogo na ukosefu wa vipaumbele katika taasisi hizo.

Akitoa maelezo juu ya mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba alitaja lengo hasa la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu  katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini ambayo washiriki wanayafanyia kazi, kujenga uwezo wa Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Wizara zao pamoja na kuona namna bora ya kuimarisha utendaji kazi katika taasisi za Serikali.

“Eneo la Ufuatiliaji na Tathmini limekuwa likilega leg asana katika taasisi nyingi za Serikali hivyo tumeona ni vema tukakaa pamoja kuona namna bora ya kuliimarisha,” Bw. Kiliba aliongeza.
Mafunzo hayo yameanza leo na yanahudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara 12 ambazo ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya utumishi wa Umma, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Tume ya Mipango.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
24 Novemba, 2016.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi Susan Mlawi, akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
 Baadhi ya washiriki kutoka Wizara Mbalimbali wakifuatilia mada wakati wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
 Mshiriki wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Mariam Silim akitoa neno la shukrani kwenye Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA