UJUE UTAJIRI WA RAIS MTARAJIWA WA MAREKANI DONALD TRUMP JOHN









DONALD TRUMP JOHN alizaliwa 14 Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.
Upande wa baba yake (Fred Trump aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake (Mary) ni mzaliwa wa Scottish.
Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambako alihitimu shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.
Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ambayo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu.
Trump ambaye ni baba wa watoto watano, ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.
Baadhi ya mali anazomiliki
Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama
Trump Tower lililopo Manhattan
Wollman Rink lililoko Central Park
Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey
Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland
Trump Hotel Las Vegas
Trump International Hotel & Tower ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Chicago
Trump International Hotel ya Las Vegas
Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk
Trump SoHo ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Toronto
Taasisi ya Donald J. Trump
Branding na licensing
Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.
Utajiri
Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni 3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi kwenye historia ya nchi hiyo.
Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake (brand), Trump anakadiliwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 na kuwa tajiri namba 324 wa dunia na wa 156 kwa nchi ya Marekani.
Trump ni Mwenyekiti na Rais wa Shirika Kibiashara la Trump (Trump Organization) lenye makao yake makuu katikati ya Mji wa Manhattan ambalo linamiliki majengo mengi marefu, hoteli, kasino, timu za gofu, ndege na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo nchini Marekani na nje ya Marekani.
Na John Badi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI