4x4

WABUNGE WASHITUSHWA NA KIFO CHA GHAFLA CHA MBUNGE HAFIDH ALI TAHIR

 Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Hafidh Ali Tahir wakati wa kuuaga mwili bungeni Dodoma jana. Hafidh alifariki ghafla usiku wa manane kuamkia jana na katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Hafidh Ali Tahir wakati wa kuuaga mwili bungeni Dodoma
 Wabunge wakiwa wameinama kwa dakika moja bungeni Dodoma jana, kuomboleza kifo cha mbunge mwenzao Hafidh Ali Tahir
 Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto aliyekuwa akikakaa jirani bungeni na marehemu Hafidh Ali Tahir akikusanya nyaraka za marehemu mara baada ya Spika Job Ndugai kutangaza msiba huo jana. Hafidh alikuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Bunge wakati Mwamoto ni kocha mkuu.


Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akitoa salamu za rambirambi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Hafidh Ali Tahir  wakati wa kuuaga mwili bungeni Dodoma jana. Hafidh alifariki ghafla usiku wa manane kuamkia jana na katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.
 Mbunge wa Viti Maalum, Asha Abdalah Juma 'Mshua' akiangua kilio wakati huku akifarijiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlata wakati jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar, Hafidh Ali Tahir likiwasili kwenye viwanja vya Bunge jana kwa ajili ya kuagwa na wabunge.
 Mbunge wa Jimbo la Kwembesamaki, Zanzibar, Ibrahim Raza akiangua kilio wakati jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar, Hafidh Ali Tahir likiwasili kwenye viwanja vya Bunge jana kwa ajili ya kuagwa na wabunge.
 Wapambe wa Bunge, wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa  aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Hafidh Ali Tahir  baada ya kuagwa na wabunge bungeni Dodoma

Spika wa Bunge, Job Ndugai akihuzunika wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mbunge huyo.
Post a Comment