AZAM YASAJILI 'MKATA UMEME' WA CAMEROON HATARI TUPU


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imemsajili kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo kutoka Cameroon kuchukua nafasi ya Jean Baptiste Mugiraneza wa Rwanda anayeondoka baada ya misimu miwili ya kuitumikia timu hiyo.
Pamoja na Mpondo, mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, wamemsajili beki wa kati Mghana Yakubu Mohammed, kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo na winga Joseph Mahundi.
Zoezi hilo la kuingiana mikataba limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul Mohammed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Meneja wa timu, Phillip Alando.
Wakati Mohammed, 20, amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Aduana Stars ya Ghana, utakaomuweka kwenye viunga vya Azam Complex hadi Desemba 14, 2019 akiziba nafasi ya Pascal Wawa, huku Mpondo anayetokea Coton Sports ya Cameroon, kwa upande wake akisaini mwaka mmoja.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez (kushoto) akimkabidhi jezi ya Azam FC mchezaji mpya Stephan Kingue Mpondo
Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez (kushoto) akimkabidhi jezi ya Azam FC mchezaji mpya Joseph Mahundi  
Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez (kushoto) akimkabidhi jezi ya Azam FC mchezaji mpya Yakubu Mohammed

Nyota hao wawili wamepewa rasmi mikataba baada ya kulivutia benchi la ufundi la Azam FC kwenye majaribio waliyokuwa wakifanya ndani ya kikosi hicho.
Katika kuongeza makali kwenye eneo la ushambuliaji, Azam FC imemrejesha winga wake wa zamani aliyekulia Azam Academy, Mahundi, ambaye amesaini miaka miwili akitokea Mbeya City, alipomaliza mkataba baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Azam FC tunaamini ya kuwa ujio wa nyota hao, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajia kuanza wikiendi hii, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shirikisho Afrika (CC) mwakani.
Hivyo mashabiki wa Azam FC wasiwe na wasiwasi waendelee kuisapoti timu, kwani bado uongozi wa timu kwa kushirikiana na benchi la ufundi, una nia ya dhati ya kuipeleka mbele timu kufikia kwenye mafanikio yanayokusudiwa kwa kukiboresha kikosi kadiri inavyowezekana.
Wakati huo huo, Azam FC inapenda kuweka wazi taarifa ya kufikia makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji raia wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’, ambaye amepata timu nchini Vietnam na muda wowote kuanzia sasa atakwenda huko.
Azam FC inamtakia mafanikio mema Migi huko aendako na inapenda kumkaribisha muda wowote atakapojisikia kurejea tena hapa na katika kuziba nafasi yake tumeamua kumsajili Mpondo, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Cameroon kwenye kikosi kilichoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika nchini Rwanda mwanzoni mwa mwaka huu. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*