Klabu ya China kumlipa Tevez zaidi ya pauni 310,000 kwa wiki



Shenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca JuniorsImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionShenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca Juniors
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Carlos Tevez amejiunga na klabu ya China Shenghai Shenhua ,klabu hiyo imethibitisha.
Shenghai wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya Boca Juniors lakini hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu kandarasi hiyo.
Shanghai inayofunzwa na Gus Poyet imeripotiwa kuweka kandarasi ya pauni milioni 40 ikiwemo mshahara wa zaidi ya pauni 310,000 kwa wiki.
Boca Juniors imesema: Kila la kheri Carlitos. Utakuwa myoyoni mwetu kila wakati.
Tevez alicheza kwa miaka saba katika ligi ya Uingereza na akajishindia mataji ya ligi akiwa na timu zote mbili za Manchester.
Pia alishinda taji la vilabu bingwa Ulaya akiwa na United mwaka 2008 kabla ya kujiunga na Juventus mwaka 2013, ambapo alijishindia mataji mawili ya ligi ya Itali.
Mnamo tarehe 23 mwezi Disemba Chelsea iliingia katika mkataba na Shanghai kumnununua kiungo wa kati wa Chelsea Oscar katika uhamisho utakaogharimu pauni milioni 60.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI