MABLOGA KUFANYA MKUTANO MKUU DESMBA 5-6 DAR

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008.  Kinapenda kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.
Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya NMB na wadhamini wengine unatarajia kuanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa siku mbili mfululizo.

Katika mkutano huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine.

Aidha katika mkusanyiko huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana Blogu.
Mkutano huu ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.

TBN inaendelea kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake.

Lakini kwa namna ya pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF, NHIF, SBL, na Coca Cola kwa kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya.

Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.


Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
0756469470

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI