4x4

MAHAKAMA KUU ARUSHA YAWAPA SIKU 10 MAWAKILI WA LEMA


Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya mahakama kumalizika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.


 Na.Vero Ignatus,Arusha
  
  Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo  amewapa siku kumi(10)mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema .

Agizo hilo limekuja kutokana na mahamama kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa mbunge hu


Jaji  Dkt.Modesta Opiyo  mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa lazima.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh  Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia leo,hadi hapo tar 30dec2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.

                                                          ****TUJIKUMBUSHE****
Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.
Post a Comment