Matukio yaliyovutia wengi kwa picha 2016



Chaguo letu la baadhi ya picha zilizotia fora katika kuelezea taarifa kama zilivyochukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya dunia katika kipindi cha mwaka 2016
Jackeline, mwenye umri wa miaka 26, akimbeba mwanae wa kiume aliezaliwa na maradhi ya Zika mbele ya nyumba yao katika kitongoji cha Olinda, karibu na Recife, Brazil, tarehe 11 Februari 2016.Image copyrightNACHO DOCE/REUTERS
Image captionMwanzoni mwa mwaka dunia ilikuwa katika kipindi cha dharura cha kubaini ni vipi na kwanini kirusi cha Zika kinaweza kusababisha maafa miongoni mwa watoto wachanga wanaozaliwa Amerika kusini kwa kudumaza ukuaji wa ubongo. Brazil iliripoti visa 4,000 vya maambukizi hayo tangu Oktoba 2015 - idadi ambayo haikutarajiwa. Shirika la Afya Duniani lilitangaza hali ya dharura ya kiafya katika kushughulikia maradhi hayo.
Rais wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama wakicheza densi ya tangoImage copyrightPABLO MARTINEZ MONSIVAIS/AP
Image captionRais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obam walialikwa kujaribu kucheza densi ya taifa la Argentina , tango,katika dhifa ya kitaifa walipokuwa ziarani nchini humo mwezi Machi
Muandamanaji akikamatwa na polisi kwa kupinga mauaji ya Alton Sterling aliyepigwa risasi karibu na kituo cha makao makuu ya polisi cha Baton Rouge Police huko Baton Rouge, Louisiana, USA, tarehe 9 Julai 2016.Image copyrightJONATHAN BACHMAN/REUTERS
Image captionIeshia Evans, mwenye umri wa miaka 27- ambaye ni muuguzi kutoka New York, alikuwa kama kielelezo cha utetezi wa haki za maisha ya watu weusi baada ya picha yake kusambazwa .Ilichukuliwa tarehe 9 Julai alipokuwa akiandamana mjini Baton Rouge kupinga mauaji ya polisi dhidi ya watu weusi.
Mwanamume aliyechuruzika damu akiwa amesimama kwenye daraja la Bosphorus huku wanajeshi wa Uturuki wakikabiliana na watu kwenye lango la kuingilia kwenye daraja mjini Istanbul tarehe 16 Julai 2016Image copyrightBULENT KILIC/AFP
Image captionWakati wa jaribio la mapinduzi lililofeli , daraja la Bosphorus mjini Istanbul lilikuwa eneo la malumbano baina ya wanajeshi wakijaribu waliofanya jaribio la mapinduzi, serikali na wafuasi wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Juhudi za kupigania eneo hilo lenye muhimu linalounganisha Ulaya na Asia zilisababisha kuibuka kwa mapigano makali baina ya pande mbili.
Watu wakitembea kwenye daraja la vioo la Zhangjiajie, katika mkoa wa Hunan , China, tarehe 1 Agostu, 2016.Image copyrightREUTERS
Image captionNjia ya vioo iliyoko inayozunguka kilima cha Tianmen mjini Hunan ilikuwa ni mojawapo ya vitu vya kushangaza vilivyowavutia watalii nchini Uchina. Njia hiyo vya vioo ilikuwa na urefu wa mita 100 . Kwa wale wasio na uoga wa kutembea kwenye njia hiyo, ni mahala pazuri pa kupata taswira nzima ya maeneo yote ya Hunan
Umati wa watu wakikusanyika mbele ya picha ya muimbaji David Bowie aliyejulikana kama Jimmy C, mjini Brixton, kusini mwa London.Image copyrightTIM IRELAND/AP
Image captionPicha ya David Bowie iliyokuwa kumbu kumbu ya mwanamuziki huyo baada ya kifo chake inatarajiwa kuorodheshwa katika samani za manispaa ili kuhakikisha inatunzwa kwa muda mrefu . Umati wa mashabiki wake walikusanyika mjini Brixton kusini mwa London, eneo alikozaliwa Bowie kusherehekea maisha na muziki wake Muimbaji huyo mwenye ushawishi alifariki kwa maradhi ya saratani tarehe 11 Januari akiwa na umri wa miaka 69.
Beyonce akicheza wimbo wake Freedom pamoja na Kendrick Lamar katika tuzo la Black Entertainment Television (BET) mjini Los AngelesImage copyrightDANNY MOLOSHOK/ REUTERS
Image captionBeyonce akizindua kipindi cha tuzo la Black Entertainment Television (BET) Awards mjini Los Angeles kwa onyesho la muziki la kushtukiza la wimbo wake Freedom pamoja na Kendrick Lamar, akidensi kwenye dimbwi la maji, alishinda tuzo la video ya mwaka na la chaguo la watazamaji kwampangilio wa wimbo wake, lakini alikuwa tayari ameisha ondoka kuelekea London kwa tamasha kwa hiyo mama yake Tina Knowles alipokea tuzo kwa niaba yake.
Wahamiaji kutoka Eritrea,wakiruka ndani ya maji kutoka kwenye mtumbwi wenye umati wa watu wakisaidiwa na shirika moja lisilo la kiserikali kaskazini mwa mji wa Sabratha, Libya, tarehe 29 Agosti 2016.Image copyrightEMILIO MORENATTI/AP
Image captionTakriban wahamiaji 3,800 wamefariki ama kutoweka katika bahari ya Mediterranean mwaka 2016 - mwaka mbaya wa vya wahamiaji kuwahi kushuhudiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) limesema . Hii ilitokea licha ya kupungua kwa idadi ya wakimbizi wanaovuka bahari hiyo ikilinganishwa na 2015, ambapo vifo 3,771 viliripotiwa. Hapa wahamiaji , wengi wao kutoka Eritrea, wakiruka ndani ya maiji wakati wa operesheni ya uokozi kaskazini mwa Sabratha, Libya.
Abbey D'Agostino wa United States (kulia)akisaidiwa na Nikki Hamblin wa New Zealandbaada ya kuanguka katika mbio za mita 5,000m- wanawaketarehe 16 Agosti 2016 mjini Rio de Janeiro, Brazil.Image copyrightIAN WALTON/GETTY IMAGES
Image captionWakimbiaji wawili katika Olimpiki mjini Rio walisifiwa baada ya kusimama kusaidiana baada ya wanawake wote kuanguka chini wakati wa mbio za mita 5,000. kwa wanawake. Mkimbiaji wa Marekani Abbey D'Agostino akimtia moyo mkimbiaji wa d New Zealand Nikki Hamblin alipkuwa ameanguka wakati wawili hao walipogongana . Licha ya kwamba D'Agostino alionekana akichechemea ,aliweza kukimbia hatua chache baada ya kumsaidia Hamblin kuinuka kabla ya kuanguka , huku mNewsealand akirudisha shukrani kwa kumsaidia hasimu wake.
Usain Bol wa Jamaica akikamilisha mbio za mita 100mwanaume katika Olympiki mjini Rio 2016.Image copyrightCAMERON SPENCER/GETTY IMAGES
Image captionMkimbiaji maarufu wa Jamaica Usain Bolt alipata fursa ya kutabasamu mbele ya kamera huku akipata ushindi wa mbio za nusu fainali mita 100. Ni tukio lililopata umaarufu katika mitandao. Baadae alishinda finali kwa muda wa sekunde 9.81 -taji lake la tatu la mita 100 Olimpiki.
Omran Daqneesh mvulana wa Syrian aliyejaa vumbi na damu akiwa amekaa ndaniya gari la kubebea wagonjwa aliokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lililopigwa na makombra ya anga katika mji wa ngome ya waasi wa Syria wa Qaterji tarehe 17 Agosti 2016.Image copyrightMAHMOUD RSLAN/AFP
Image captionPicha ya mateso na umwagaji damu ya mtoto wa kiume wa Syria aliyeokolewa kutoka kwenye jengo lililoharibiwa mjini Aleppobaada ya mashambulio ya anga iliibua hisia kali kote duniani watu wengi wakilaani yanayoendea nchini Syria. Picha ya mvulana ambaye alitambulishwa kama Omran Daqneesh mwenye umri wa miaka mitano, aliyeketi kwenye ambilansi ilitolewa na wanaharakati na kuenezwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wanaume wa Syeia waliowabeba watoto wao wachanga wanaolia wakitoroka majengo yaliyolipuliwa kwa makombora ya anga kaskazini mwa mji wa Aleppo tarehe 11 Septemba 2016.Image copyrightAMEER ALHALBI/AFP
Image captionFamilia zilitafuta njia za kutorokea upitia majengo yaliyoporomoka kufuatia mashambulio ya anga mjini Alleppo tarehe 11 Septemba. mkataba wa usitishaji mapigano ulitarajiwa kufungua njia kwa ajili ya watoaji wa misaada ndani ya Syria, lakini Urusi iliishutumu Marekani kwa kushindwa kutimiza wajibu wakechini ya mkataba huo.
Mwezi ukiangazia juu ya eneo la Uppatasanti Pagoda huko Naypyitaw, nchini Burma, tarehe 14 Novemba 2016.Image copyrightHEIN HTET/EPA
Image captionMwezi ulikaribia dunia tukio ambalo halikuwahi kushudiwa tangu mwaka 1948. Watu mbali mbali walikusanyika katika maeneo mbali mbali ya dunia kushuhudia tukio. Mwezi huo The "supermoon" ulikuwa na mwangaza zaidi barani Asia tarehe 14 Novemba.
All photographs are copyrighted.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI