MAZISHI YA KIHISTORI IRINGA MAREHEMU AZIKWA KABURI MOJA NA KONDOO



 Wanafamilia   wakiwa   wamelizungika kaburi la marehemu Ngaga  aliyezikwa kaburi  moja na kondoo pamoja na  kuku mweusi  leo kwenye  kitongoji cha Mkawaganga kijiji  cha Mbigili  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa 
  Mganga  wa  kienyeji  Galasiano  Nyenza (kulia)  akiwa na mtoto wa marehemu  Andrea Ngaga  ,Kurugenzi Ngaga  kushoto  baada ya  kufanyika kwa mazishi ya kimila  katika  kijiji  cha Mbigili Kilolo kwa marehemu kuzikwa kaburi moja na kondoo na kuku  mweusi 
 Mganga  Nyenza aliyeongoza mazishi hayo katikati  akiwa na baadhi ya ndugu kando ya kaburi 
 Waombolezaji  wakitoka kuzika 
                                                      Marehemu  enzi  za uhai  wake 
Nyumbani kwa marehemu   waombolezaji  wakiwa  kwenye  foleni 
....................................................................................................
                              Na MatukiodaimaBlog
MAMIA  ya  wakazi  wa kijiji  cha  Mbigili na  mji  wa Ilula  katika  wilaya ya  Kilolo  wamefurika katika mazishi  ya aina  yake  yaliyofanyika katika kitongoji  cha Mkawaganga  kijiji  cha Mbigili  wilaya ya  kilolo mkoani Iringa  kushuhudia mazishi hayo ya  kihistoria baada ya mzee mmoja aliyefariki  dunia ghafla  kuzikwa kaburi  moja na kondoo pamoja na   kuku mweusi.

Tukio   hilo  limetokea  leo  wakati  wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90) mkazi wa kitongoji  cha Mkawaganga  aliyekuwa  akijishughulisha na kazi  za uganga  wa kienyeji kijijini  hapo enzi  za  uhai  wake .

Baadhi ya  wananchi  waliofika katika mazishi  hayo  walisema  kuwa  walilazimika  kusitisha   shughuli  zao za  shamba na biashara na  kufika  kushuhudia  mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza  kufanyika katika  kijiji  hicho  alisema  John  Mfaligoha  kuwa  kabla ya  kifo marehemu  huyo  alipata  kuwaeleza  aina ya mazishi yake  yatakavyokuwa .

Hivyo alisema  wananchi   waliowengi   walifika  kutaka  kushuhudia tukio  hilo la mazishi  na  ndio  sababu  iliyopelekea  wananchi kusukumana msibani  wakati wa mazishi  kwa  kila mmoja kutaka  kushuhudia  tukio  hilo la kihistoria katika kijiji   hicho.

Mwenyekiti  wa  serikali ya  kijiji  cha Mbigili  Ibrahim  Rashid (46)  alisema  amezaliwa katika  kijiji  hicho  tukio hilo ni la kwanza  kufanyika hajapata  kushuhudia mazishi ya  aina  hiyo   zaidi ya  kusikia katika vyombo  vya habari  kutoka nje ya  kijiji  chake na  kuwa  mazishi hayo  yamefanyika kimila  zaidi na kimsingi  huwa marehemu anachagua mtu  wa  kuzikwa nae  kabla ya  kifo .

Ila hakuweza  kuacha maagizo zaidi ya  kuomba pindi atakapokufa kuzikwa kimila na ndio  sababu  aliyeongoza  mazishi hayo ni mganga  wa kienyeji  kutoka Ifunda  wilaya ya  Iringa  Galasiano Mfaume Nyeza  ambae  ni baba mdogo  na marehemu  huyo .


Mtendaji  wa serikali ya  kijij  hicho cha Mbigili Thabith  Kalolo  alisema  kuwa kimsingi  hakuna  kosa  lolote  familia ambalo  wamelifanya kwa  kufanya mazishi ya  aina  hiyo  kwani serikali haiingilii uhuru wa  wananchi  wake kuamini masuala ya  mila na kuwa   iwapo mazishi hayo yangekiuka haki  za  binadamu mwingine mfano  kama wangekata  kumzika  marehemu na  binadamu mwingine aliyehai hapa isingewezekana  ila  kwa kumzika na kondoo na kuku  mweusi hakuna  shida .

Hata   hivyo  alisema tofauti  ya  rekodi ya misiba iliyopata  kutokea  katika  kijiji  hicho ,msiba wa mganga  huyo  umevunja rekodi kwa  kuhudhuriwa na idadi kubwa ya  watu  na kuwa   msiba uliovunja rekodi kwa michango ni huo pekee  kwani  misiba mingine fedha za rambi rambi   huwa ni kati ya Tsh 300000 hadi 500000 mwisho  ila msiba  huo rambi rambi ni  zaidi ya Tsh milioni 1.3

Mtoto  wa marehemu  Kurugenzi Ngaga  alisema  kuwa babake  alifariki  dunia juzi  Desemba 20 majira ya  saa 6 usiku mwakla huu kuwa  alikuwa  akisumbuliwa na tatizo ya chembe  ya Moyo  na kuwa ameacha   wajane   wawili na watoto 19.

Kurugenzi alisema  kimila kama  ingekuwa  zamani  marehemu  angezikwa na mjukuu wake  aliyemteua kushika mikoba yake  ila  kutokana na mambo  ya mila kwa  sasa kupewa kisogo waliona ni  vema wakamzika na kondoo na kuku  huyu  mweusi .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*