MWANAFUNZI AFA MAJI AKIOGELEA HOTEL YA MOUNT MERU ARUSHA


Mount Meru Hotel
Mwanafunzi  wa darasa la tano  shule ya msingi ya Sekei iliyopo
halmashauri ya Arusha DC wilayani Arumeru Criff Laiza (12), amekufa
maji wakati akiogelea kwenye  bwawa la maji yenye kina kirefu katika
hotel ya kitalii ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha .
 

Tukio hilo limetokea Desemba 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni
wakati marehemu na watoto wengine wakiogelea katika hotel hiyo ikiwa
ni sehemu ya kusheherekea sikukuu ya X-mass .
 

Kaimu Meneja wa Hotel ya Mount Meru, Eric Mgenya akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na atalitolea ufafanuzi
baada ya polisi kukamilisha upelelezi wa tukio hilo.
 

Alisema  baada ya kutokea uongozi wa hotel hiyo, walitumia gari aina
ya Noah lenye namba T.883 DJM pamoja na gari dogo lenye namba T.445
BSC aina ya Toyota Corrola walipakia mwili wa marehemu kwa lengo la
kuokoa uhai wake na walipofika katika hospital ya Aicc na mwili huo
kupimwa waliarifiwa kuwa tayari marehemu alishafariki kitambo.
 

Baadhi ya watoto  waliokuwa wakiogelea na marehemu  katika hotel hiyo
walisema, marehemu Laiza alihama ghafla kwenye bwawa la watoto na
kwenda kuogelea bwawa  linalotumiwa na watu wazima ambalo wakati huo
hapakuwa na mtu yoyote akiogelea, lakini ghafla hakuonekana tena hadi
alipo kutwa ameelea juu ya maji .
 

Kwa upande wake Babu wa mtoto huyo Emanuel Meage alisema tukio hilo
limeshtua sana, kwani  mjukuu wake aliaga kuwa anaenda kuogelea katika
hotel hiyo na wenzake hata hivyo alishangaa kupata taarifa za mjukuu
wake kufa maji.
 

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wazazi  ambao hawakutaka kutaja
majina yao wameutupia lawama uongozi wa hotel ya hiyo kwa kushindwa
kuwa na usimamizi mzuri na ulinzi wa watoto hao, badala yake wamekuwa
wakijali kukusanya fedha ya kuogelea na kuwaacha watoto wafanye
wawezavyo kitendo ambacho sio sahihi wakidai kuwa eneo hilo ni hatari
na  sio salama kwa mazingira ya mtoto .
 

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo alithibitisha tukio
hilo na kueleza kuwa polisi wapo katika hatua ya uchunguzi na
atalitolea ufafanuzi, mara baada ya uchunguzi kukamilika na hakuna mtu
yoyote hadi sasa anashikiliwa kutokana na tukio hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI