Mwanzilishi wa JamiiForums Asomewa Mashtaka 3 Kisutu, 2 Apata Dhamana, Apelekwa Gereza la Keko


melo
Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo ameshtakiwa kwa makosa matatu likiwemo la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini kinyume cha sheria.
Makosa mengine mawili aliyoshtakiwa Melo ni kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao.
Katika mashtaka hayo matatu aliyosomewa, mawili amepata dhamana.
Imeelezwa kuwa Melo ameshindwa kukamilishiwa dhamana ya shtaka la tatu na mwendesha mashtaka, hivyo amepelekwa Gereza la Keko kinyemela na uenda akarudishwa mahakamani Jumatatu ijayo.
Tayari wadhamini wa shtaka la tatu walikuwa wamepatikana ndani ya muda lakini upande wa Jamhuri ulikuwa umeshaondoka mahakamani hapo maana kwa kawaida mahabusu hupelekwa gerezani saa nane mchana.
Aidha imeelezwa kuwa tofauti na utaratibu uliozoeleka, Maxence Melo kaondolewa kinyemela pasipo mawakili wake wala ndugu zake kujua na kupelekwa Gereza la Keko majira ya saa tano asubuhi.
Mashtaka ya Melo haya hapa;
mashtaka-melo-3
mashtaka-melo-1
mashtaka-melo-2
Aunt Ezekiel: Siku ya Kwanza Kufanya Mapenzi na Moze Iyobo, Tulikuwa Tunaangalia TV

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.