NEC YAFANYA USAILI KUWAPATA MRATIBU NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI, ZANZIBARMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti cha Usaili wa kuwapata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani, Zanzibar . Uchaguzi huo utakaofanyika Januari 22, 2017.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume wakati wa kikao cha Usaili wa nafasi ya Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjata.

Baadhi ya Wajumbe wa Seckretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakifuatilia kwa makini zoezi la Usaili wa kuwapata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipitia vyeti na nyaraka mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Usaili wa nafasi ya Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakiendelea na zoezi la Usaili kwa waombaji wa nafasi Mraratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.


Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Mratibu wa Mkoa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bw. Salum Juma Mgunya akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini Zanzibar.

Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Msimamizi wa Uchaguzi  katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bi. Fatma Gharib Haji akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini


Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia zoezi la Usaili la kumpata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Dimani Zanzibar. PICHA/ Aron Msigwa – NEC.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)