Rais Magufuli ateua wenyeviti 7 wa bodi na Wajumbe wa Baraza



jpm5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Wenyeviti 7 wa Bodi za Taasisi za Serikali, na pia ameteua Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania na Mjumbe mmoja wa Baraza la Taifa la Biashara.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 19 Desemba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;
  1. Rais Magufuli amemteua Bw. Ali Mufuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira.
Bw. Ali Mufuruki ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Infotech Investment na Mwenyekiti wa Taasisi ya Afrika inayojihusisha na uendelezaji wa vipaji vya uongozi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
  1. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Christopher Kajolo Chiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Mhandisi Christopher Kajolo Chiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sabetha Mwambenja ambaye amemaliza muda wake.
  1. Rais Magufuli amemteua Bw. Peter M. Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Bw. Peter M. Maduki anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Idrissa Mshoro ambaye amemaliza muda wake.
  1. Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Dkt. Yamungu Kayandabila ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Peter Ilomo ambaye amemaliza muda wake.
  1. Rais Magufuli amemteua Prof. Godwin Daniel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Huduma za Fedha na Mikopo (UTT-MFI)
Prof. Godwin Daniel Mjema ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Fadhili D. Mbaga ambaye amemaliza muda wake.
  1. Rais Magufuli amemteua Kepteni Ernest Mihayo Bupamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Bahari (DMI)
Kepteni Ernest Mihayo Bupamba ni Mwendesha Meli Mkuu (Principal Captain) Katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  1. Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce S. Hepelwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Miradi ya Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID)
Dkt. Aloyce S. Hepewa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. John Jingu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Tanzania. 
Dkt. John Jingu ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Dkt. Rashid Adam Tamatama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI).
 Dkt. Rashid Adam Tamatama ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Pia, Rais Magufuli amemteua Bibi. Zuhura Muro kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (Tanzania National Business Council – TNBC).
Bibi. Zuhura Muro ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi inayojihusisha na huduma za ushauri wa ubora na mafunzo (Service Limited) katika ofisi zake za Dar es Salaam. 
Wateule wote waliotajwa hapo juu, uteuzi wao umeanza tarehe 17 Desemba, 2016 
 Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Dar es Salaam, Bw. Gerson Msigwa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*