RIDHIWANI AINYOOSHEA KIDOLE SERIKALI UNYAMA WAUFANYAO WAFUGAJI,WAKULIMA


Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi aliyechomwa Mkuki na wafugaji wa kwanza kushoto.


Kwanza niruhusu nikupe Pole ndugu yangu kwa lililokukuta. La msingi Serikali inatakiwa kujua, tunaposema maoni yetu pale Bungeni tunamaanisha. yako mambo unaweza yafanyia utani lakini hapa tulipofika si kwa kuchukulia mzahamzaha. 

Waziri muhusika haya hauyaoni au niliposimulia juu ya Wananchi wa Jimbo la Chalinze kupigwa , kuvunjwa migongo na mwengine kupigwa mshale wa goti na kumpa ulemavu wa maisha mlidhani natania. Sasa hili liwe fundisho. Serikali ni lazima ije na majibu sahihi juu ya kunusuru vita ya wenyewe kwa wenyewe .

Jana mtu kavunjwa mgongo, mwengine mlemavu leo kapigwa mkuki wa mdomo umetokea shingoni. Lini tutasikia kilio hiki? Serikali sikieni kabla Damu ya watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo chao hawajapotea. Kuna sheria, na mipango ya matumizi bora ya Ardhi. Nini kinafichwa? 

Binafsi Nalaani Vitendo hivi na kuiasa Serikali yangu kujipanga vizuri kabla mambo hayajaharibika. yalianza Kilosa, Mvomelo, Chalinze, Handeni,Kiteto na sasa Mikumi ( kutaja maeneo machache) .Serikali jipangeni, kabla hapajachafuka.

RIDHIWANI KIKWETE
MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU