RIDHIWANI ATAKA KAZI ZA WASANII ZITAMBULIWE NA KUPATA FAIDA


Mbunge wa Jimbo la Chalinze RIDHIWANI KIKWETE (pichani kulia), amesema anataka kuona Wasanii Watanzania kazi zao zinatambuliwa na kuona faida ya kazi wanazofanya.

            Aidha amesema yeye kama Mbunge Kijana, anapenda kuona Wanamuziki wa Tanzania wakifanya vizuri na kuona faida ya kazi zao na kukuza soko la Muziki wao Kimataifa.

          Mbunge huyo amesema hayo alipokua Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Video ya mwanamuziki Belle 9 ya muziki wake mpya unaoitwa Give It To Me ambao amemshirikisha mwanamuziki G Nako.

          Akizungumza katika Uzinduzi huo, amesema anapenda kuona muziki wa Tanzania na wasanii wake kazi zao zikitambulika na pia waone faida ya kazi wanayoifanya. 

          Katika Uzinduzi huo amesema amejitoa kumsaidia Msanii Belle 9 kutokana na uwezo wake wa Kuimba na kipaji alichonacho.

          Ameongeza kuwa yeye ni Mbunge kijana anayetaka kuona wasanii Watanzania kazi zao zinatambuliwa na kuona faida ya kazi wanazofanya.

          Aidha ameupongeza uongozi mzima wa Vitamin Music kwa kufanikisha tukio hilo na kusema wimbo wa Give It To Me bila shaka, unaongeza idadi ya nyimbo zitakazokuwa maarufu kwenye Klabu za Tanzania.

          Ameeleza kwamba anafurahi kuona wasanii wanaanza kuondoa ile imani kuwa Bongo Flava ni muziki wa kusikiliza zaidi, na kusema ndio maana unakuta hafla mbalimbali ikiwemo Harusi au mashindano kama Miss Tanzania, zinajaa Playlist za nyimbo za Nigeria.

          Aidha amepongeza Wanamuziki kwa hatua yao ya kufikiria kuweka ‘fusion’ za muziki wa Asili kwenye nyimbo zao ili kuzipa ‘Utanzania’ unaoliliwa kila siku.

          Amesema Wimbo huo wa Belle 9 una Video nzuri na anaamini itamfikisha Belle sehemu ambazo bado hajafika. 
Sent from my iPhone

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.