Samatta ameifungia magoli mawili KRC Genk dhidi ya Waasland-Beveren


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren.
Samatta akiwa na KRC Genk katika uwanja wa ugenini amefanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 15 goli la pili dakika ya 42 kabla ya mnigeria Wilfred Ndindi kufunga goli la tatu dakika ya 80.
Wenyeji wa mchezo huo Waasland-Beveren walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi dakika ya 89, kupitia kwa mchezaji wao Zinho Gano, huo ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Croky.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*