SAMIA AWATAKA WANA CCM MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KUIMARISHA USHIRIKIANO


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akizungumza na Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni. 
Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya wakimsikiliza Mlezi wa CCM mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.
 Naibu Katibu Mkuu  CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai akihimiza Umoja na Mshikamano kwa Viongozi wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa kikao cha kupokea tathmini ya uchaguzi wa mwaka 2015 kikao ambacho mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.


                      .....................................................................................................

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM- Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama na viongozi wa CCM katika mkoa Kaskazini Unguja wadumishe na kuimarisha ushirikiano miongoni mwao kama hatua ya kujenga chama imara.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kaskazini (B) Unguja wakati akizungumza kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho kwa ajili ya kujadili mipango na mikakati ya kuimarisha chama hicho.

Mjumbe huo amesisitiza kuwa kama viongozi wa chama hicho watadumisha ushirikiano na kuondoa tofauti zao watakijenga chama na kuongeza idadi kubwa ya wanachama wapya ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa katika eneo hilo.
Amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kazi iliyopo kwa sasa kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote ni kuweka wanaweka mipango na mikakati madhubuti itakayoweza chama hicho kuendelea kushika dola.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM-Taifa  SAMIA SULUHU HASSAN ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja amesema anaimani kubwa kuwa kuanzia sasa viongozi hao watajipanga ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Kuhusu uimarishaji wa jumuiya za Chama hicho, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja waimarishe jumuiya hizo ili ziweze kutekeleza majukumu ya kichama katika kila ngazi.

Mjumbe huyo ameonya viongozi hao waache tabia ya kugombania madaraka kwenye chama bali washirikiane katika kuongeza idadi ya wanachama hasa vijana ndani ya Chama hicho.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS