SIMBA YAWAKOMBOA NYOTA WAKE WA KIGENI


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imesema kwamba imefanikiwa kuwapatia vibali vyote vya makocha na wachezaji wake wa kigeni na kehso watakuwa kazini Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online leo kwamba wamefanikiwa kukamilisha taratibu zote za kuwahalalisha wachezaji wao na makocha wa kigeni kuendelea na kazi nchini.
“Tumefanikiwa kukamilisha taratibu zote na hivi ninavyozungumza na wewe, tayari wachezaji wote wana vibali vya kufanya kazi nchini,”amesema Kahemele ambaye jana kwa pamoja na Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit na Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba walishikiliwa kwa saa kadhaa Idara ya Uhamiaji kwa kuhojiwa juu ya makosa ya kuwafanyisha kazi nchini wageni wake ambao hawakuwa na vibali.
Method Mwanjali wa Simba (kushoto) amepatiwa kibali cha kufanya kazi nchini

Kwa pamoja wote walikamatwa kwa tuhuma za kuwaruhusu wachezaji na makocha wao wa kigeni kufanya kazi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki bila na vibali, lakini Uhamiaji ikagundua ni Simba pekee ambayo wachezaji wake wote na makocha hawana vibali.
Uhamiaji ikaiagiza Simba kutowatumia makocha wala wachezaji hao bila kuwapatia vibali kwanza. Hao ni Kocha Mkuu, Mcameroon, Joseph Omog, Mganda Jackson Mayanja kocha Msaidizi, Kocha wa makipa, Mkenya Idd Salim na wachezaji Janvier Besala Bokungu kutoka DRC, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, Daniel Agyei, James Kotei kutoka Ghana, Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Laudit Mavugo kutoka Burundi. 
Simba SC inatarajiwa kushuka dimbani keshokutwa kumenyana na JKT Ruvu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ikitoka kuuanza vizuri mzunguko wa pili kwa ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Na ni mchezo huo ambao ulisababisha viongozi wa Aza, Simba na Yanga wakakamatwa Jumatano, kwa sababu Ndanda FC waliilalamikia Simba kutumia wachezaji wa kigeni ambao hawakuwa na vibali.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)