TUNDU LISSU AHOJIWA POLISI KWA SAA 6

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), ameitwa kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuhojiwa kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari wiki iliyopita kuhusu kupotea kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, Ben Saanane.

Akizungumza na JAMBOLEO jana baada ya kuwepo taarifa za kukamatwa kwake, Lissu alisema: “’Sijakamatwa ila nimeitwa leo saa 2 asubuhi lakini nimefika hapa Polisi saa 4 asubuhi nimekaa hadi muda huu saa 10.15, nimehojiwa mambo mawili.’’

Alisema amehojiwa kuhusu kauli aliyoitoa kwenye mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita akituhumiwa uchochezi kutokana na kauli kwamba kuna watu waliokamatwa sehemu mbalimbali na kuletwa Dar es Salaam na kufungiwa Mikocheni na kuteswa.

Alisema jambo la pili ni kuhojiwa kama shahidi kama ana taarifa zozote kuhusu kupotea kwa Saanane na baada ya mahojiano walimwacha wakimweleza kuwa endapo wakimwitaji watamwita.

Awali kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Lissu alisema Chadema haijui aliko Saanane na kuiomba Serikali ieleze mahali alipo kwani ina jukumu la kulinda raia.

"Chadema haijui aliko Saanane, haonekani kokote, katika mazingira haya ni vema Serikali ikaeleza kama vyombo vya ulinzi vinamshikilia na kama havijamkamata, Mamlaka husika za mawasiliano zieleze mara ya mwisho alifanya mawasiliano lini, wapi na nani maana ndio wenye uwezo wa kuamuru mashirika ya mawasiliano kusema,” alisema Lissu.

Alisema wiki mbili kabla ya Saanane kupotea kutokana aliandika katika mitandao ya kijamii akihoji uhalali wa shahada ya tatu ya Rais John Magufuli, ambapo alipokea vitisho.

Alisema hatua hiyo ilikuja baada ya Rais kuanzisha mchakato wa uhakiki wa vyeti kwa watumishi ambapo yeye aliliendeleza kwenye mitandao ya kijamii.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI