4x4

VIONGOZI SIMBA NA YANGA WAKAMATWA KWA KUTUMIA WAGENI BILA VIBALI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
IDARA ya Uhamiaji leo imewakamata viongozi wa klabu za Azam, Simba na Yanga kwa makosa tofauti ya kuajiri na kuwatumikisha wageni bila kuwa na vibali.
Habari za ndani ambazo Bin Zubeiry Sports – Online imezipata zinasema kwamba waliokamatwa ni Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba na Makatibu Wakuu wa Simba, Patrick Kahemele na Yanga Baraka Deusdedit.
Kwa pamoja wote wanakabiliwa na tuhuma za kuwaruhusu wachezaji na makocha wao wa kigeni kufanya kazi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki bila na vibali.
James Kotei alicheza bila ya kuwa kibali cha Uhamiaji mwishoni mwa wiki Mtwara

Upande wa Azam wanaodaiwa kucheza bila kuwa na vibali ni beki Yakubu Mohammed, washambuliaji Yahaya Mohammed, Samuel Afful wote kutoka Ghana na kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo kutoka Cameroon.
Kwa Simba wanaodaiwa kucheza bila kuwa na vibali ni kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, wakati Yanga inatuhumiwa kuwatumia makocha wake, George Lwandamina na Noel Mwandila wakiwa hawana vibali.
Kiungo mpya wa Yanga, Justin Zulu hakucheza mwishoni mwa wiki na alikuwa jukwaani.

Post a Comment