Watu 34 wadadaiwa kufariki katika maandamano DR Congo


  • 22 Disemba 2016
Maandamano nchini DRC ambapo takriban watu 34 wanahofiwa kufariki kulingana na shirika la Human Rights Watch
Image captionMaandamano nchini DRC ambapo takriban watu 34 wanahofiwa kufariki kulingana na shirika la Human Rights Watch
Shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya usalama ini DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila ambaye alikataa kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku ya Jumatatu.
Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini magharibi mwa Congo.
Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.
Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.
Meya wa mji huo anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI