YANGA YA LWANDAMINA YAFA 2-0 VIKOSI VIWILI


Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABAO ya mawili mshambuliaji, Emanuel Martin yameipa ushindi wa 2-0 JKU ya Zanzibar dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jioni ya leo.
Mchezaji huyo wa zamani wa JKT Mlale, Martin alifunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akiunganisha kona iliyopigwa na Mbarouk Chande wakati la pili alifunga dakika ya 27 akimalizia pasi ya Nassor Mattar.
Baada ya mabao hayo, kocha Mzambia, George Lwandamina aliyejiunga na timu mwezi uliopita kutoka Zesco United ya kwao, alimtoa beki Pato Ngonyani na kumuingiza Andrew Vincent ‘Dante’.
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akipiga mpira mbele ya kipa wa JKU, Mohamed Abrahaman leo Uwanja wa Uhuru

Katika kipindi hicho, Yanga walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga, kwanza dakika ya 14 baada ya winga Geoffrey Mwashiuya kupiga mpira wa adhabu vizuri, lakini ukadakwa na kipa wa JKU Mohamed Abrahaman na ya pili dakika 21 winga Mmalawi, Obren Chirwa alipopiga shuti kali likatoka nje.
Kipindi cha pili, kocha mpya, Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila, wazalendo Juma Mwambusi na kocha wa makipa Juma Pondamali alibadilisha wachezaji 10.
Ally Mustafa 'Barthez' alimpisha Deogratius Munishi 'Dida', Hassan Kessy alimpisha Juma Abdul, Oscar Joshua alimpisha Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' alimpisha Vincent Bossou, Said Juma alimpisha Justin Zulu, Juma Mahadhi alimpisha Thabani Kamusoko, Matheo Antony alimpisha Donald Ngoma, Obrey Chirwa alimpisha Simon Msuva, Malimi Busungu alimpisha Amissi Tambwe na Geoffrey Mwashuiya alimpisha Deus Kaseke.
Pamoja na mabadiliko hayo, Yanga haikufanikiwa kupata japo bao la kufutia machozi mbele ya timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).
Lakini angalau jitihada zilionekana na lango la JKU lilitiwa misukosuko na kama si uhodari wa kipa wa timu hiyo ya Ligi Kuu ya Zanzibar, Yanga wangepata mabao. 
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez'/Deogratius Munishi 'Dida' dk46, Hassan Kessy/Juma Abdul dk46, Oscar Joshua/Mwinyi Hajji Mngwali dk46, Pato Ngonyani/Andrew Vincent 'Dante' dk31, Nadir Haroub 'Cannavaro'/Vincent Bossou dk46, Said Juma/ Justin Zulu dk46, Juma Mahadhi/Thabani Kamusoko dk46, Matheo Antony/Donald Ngoma dk46, Obrey Chirwa/Simon Msuva dk46, Malimi Busungu/Amissi Tambwe dk46 na Geoffrey Mwashuiya/Deus Kaseke dk46.
JKU: Mohamed Abrahaman, Hafidhi Ally, Edward Mazunga, Khamis Abdallah, Issa Haidary, Fesail Salum, Mabrouk Chande, Is Haka Othumani, Nasoro Mattar, Emmanuel Martin na Mohammed Abdallah.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA