Dkt. Tulia Aongoza Mkesha wa Mwaka Mpya Dar


1
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipeperusha bendera ya Tanzania kuashiria kuukaribisha mwaka 2017 baada ya kusalia dakika moja kabla ya kuingia mwaka mpya.
2
Mchungaji wa Kanisa la TFSC la Sinza, Eden Geofrey,  akisali mbele ya wananchi waliofika katika mkesha huo
3
Baadhi ya wachungaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo wakijitambulisha katika Mkesha wa Mwaka Mpya 2017.
4
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkesha huo.
5
Askofu Emmanuel Malisa akicheza kwa furaha.
6
Hali ilivyokuwa baada ya kutimu saa 6:00 usiku.
7
Kikundi cha kusifu na kuabudu kikiwa katika maombi.
8
Wananchi wakifurahia mkesha huo.
10
Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Lyapinda, mkazi wa Temeke Mikoroshini (aliyeko mbele) akicheza kwa furaha baada ya kuumaliza mwaka 2016.
NAIBU Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson,  usiku wa kuamkia leo, amewaongoza Watanzania  katika Mkesha wa Mwaka Mpya uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkesha huo ulioandaliwa na makanisa ya Kikristo kwa kuwashirikisha wachungaji mbalimbali chini ya mwenyekiti wao, Askofu Godfrey Emmanuel Malisa,ulikuwa na lengo la kuliombea taifa amani.
Mbali na hilo, mkesha huo ulikuwa na lengo la kutoa shukrani kwa utendaji mzuri wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa utendaji mzuri na nia njema ya kujenga  Tanzania mpya.
Dkt. Tulia alisema sasa ni wakati wa kila Mtanzania kurudi katika njia sahihi impendezayo Mungu na kujenga jamii yenye tija katika kumcha Mungu.
Stori: Denis Mtima na Ally Katalambula/GPL
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA