Jamaa walivyotapeli wateja 400 kwa kuanzisha benki bandia China


Leo January 06 2017 habari iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa imeeleza kuwa mahakama mjini Nanjing, China, imewafunga jela wanaume wawili waliowatapeli wateja kupitia benki bandia.
Watu hao waliotambuliwa kwa majina Zeng na He, walipatikana na makosa ya kujipatia yuan Dola milioni 63 sawa na takribani  Bil 136.6 kutoka kwa wateja 400, wamefungwa jela miaka tisa. 
Imeelezwa walianzisha chama cha ushirika ambacho ofisi yake ndani zilifanana na za benki moja inayomilikiwa na serikali, walikuwa na madawati na makarani wenye sare zilizofanana na makarani rasmi wa benki ya serikali. Hata stakabadhi za kuweka amana ya pesa kwenye benki zilikuwa sawa na za benki ya serikali.
Ingawa taasisi hiyo ilikuwa na kibali cha kuhudumu kama chama cha ushirika, haikuwa na kibali cha kuhudumu kama benki. Wahudumu waliwavutia wateja kwa kuwaahidi viwango vya juu vya riba kwa pesa walizoweka amana.
fake-bank-in-china-nanjing-mou-village-economic-cooperation-unit-inside-banking-hall
Shughuli haramu za taasisi hiyo ziligunduliwa na mfanyabiashara aliyekuwa ameahidiwa riba ya juu alipodai riba aliyoahidiwa lakini akakosa kulipwa na akatoa taarifa kwa maafisa wa polisi mwaka 2014 na baada ya hapo uchunguzi wa kina ulianzishwa.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS