Jeshi lamuunga mkono rais Jammeh nchini Gambia



Jenerali Badjie amuunga mko rais Jammeh licha ya mataifa ya magahribi kutoa vitisho vya kijeshi dhidi yakeImage copyrightAFP
Image captionJenerali Badjie amuunga mko rais Jammeh licha ya mataifa ya magahribi kutoa vitisho vya kijeshi dhidi yake
Mkuu wa jeshi la taifa la Gambia amemuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo.
Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais na Adama Barrow.
Awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo lakini akabadili nia siku kadhaa baadaye akitaja kuwepo kwa udanganyifu wa kura.
Katika barua kwa magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litamtii rais huyo.
Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.
Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.
Adama Barrow na rais Jammeh kuliaImage copyrightAFP
Image captionAdama Barrow na rais Jammeh kulia
Kundi la bwana Barrow awali lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.
Hatua hiyo ya Jeshi inaonekana kuleta utata katika kuanzisha serikai mpya baada ya Jammeh iliokuwa madarakani kwa miaka 22.
Taifa hilo dogo la Afrika magharibi halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlka kutoka uongozi mmoja hadi mwengine kwa njia ya amani tangu taifa hilo lijipatie Uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1965.
Mzozo kuhusiana na matokeo ya uchaguzi umesababisha wasiwasi, huku mataifa jirani na jamii ya kimataifa yakimtaka rais Jammeh kuondoka mamlakani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*