Kuapishwa kwa Trump: Mambo muhimu kuhusu utawala wa Trump Marekani



TrumpHaki miliki ya pichaAP
Kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa rais mteule wa Marekani pamoja na chama chake kuchukua udhibiti wa bunge la Congress, kumezua maswali chungu nzima kuhusu uchaguzi huo na ni kipi kitafuatia.
Kuanzia bima ya afya, ndoa za jinsia moja, mabadiliko ya hali ya hewa na Obamacare. Raia wa Marekani kote duniani wanataka kujua hali ya siku zao za baadaye chini ya uongozi mpya. Haya ni baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye mitandao

Trump ataingia lini rasmi madarakani?
Ataapishwa siku ya Ijumaa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 2017. Lakini tayari ametangaza maafisa wakuu wa utawala wake, amekuwa akipewa taarifa za siri zikiwemo za siri, kuhusu usalama na oparesheni za kijeshi.

Trump ataishi ikulu ya White House?

Wakati wa mahojiano na mtandao moja mwaka uliopita, Bw Trump alionekana kuzima uvumi kuwa atakiuka tamaduni ya miaka mingi ya kuishi ikulu na hata mjini Washington.
Kwenye mahojiano hayo Trump alisema kuwa bila shaka ataishi kwenye ikulu.

Trump ataendelea kusimamia biashara zake akiwa Rais?

La hasha wakili wake amesema kuwa biashara zake Trump zitasimamiwa na watoto wake, Donald Junior, Ivanka na Eric.

Trump ataanza lini kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani?

Donald Trump alilifanya suala la ujenzi wa ukuta kwenye mpaka ili kuzuia wahamiaji haramu kuwa ajenda kuu wakati wa kampeni yake.
UkutaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUkuta utajengwa pahala pa ua huu?
Makala moja katika mtandao wake inaeleza jinsi atailazimisha Mexico kulipia gharama ya ujenzi wa ukuta huo
Kutoka na gharama kubwa inayohitajika na changamoto za kupata ardhi ya kuujenga ukuta, wadadisi wanasema kuwa ukuta huo huenda usijengwe. Kile wanachotarajia ni kuboresha sera za mpaka na sheria za uhamiaji.
Bw Trump hata hivyoa amesisitiza kwamba utajengwa na ujenzi utaanza karibuni. Ingawa ameashiria kwamba huenda ufadhili ukatoka kwa serikali ya Marekani, amesisitiza kwamba Mexico lazima mwishowe itagharimia ujenzi huo.

Atasitisha utoaji mimba?

Mwezi Machi mwaka jana Donald Trump alisema kwa utoaji mimba unahitaji kuharamishwa na aliunga mkono aina fulani ya adhabu kwa wanawake ambao hutoa mimba. Lakini baadaye alionekana kulegeza kamba akisema kuwa suala hio linastahili kushughulikiwa na majimbo binafsi.
Trump amesema kuwa anaunga mkono marufuku dhidi ya utoaji mimba, isipokuwa ile inayokana na ubakaji na wakati maisha ya mama yako hatarini.

Nina bima ya afya chini ya mfumo wa Obamacare. Nitaipoteza?

Donald Trump ametaja wazi kuwa kuondoa mfumo nafuu wa Obamacare ndio itakuwa ajenda yake kuu , na anarajia kuuondoa haraka iwezekanavyo.
Matibabu Cincinnati, OhioHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY

Anaweza kuamrisha shambulio la nyuklia?
Rais wa Marekani ana mamlaka ya kuamrisha shambulizi la nuklia mwa muda mfupi, mkoba wa nyuklia au "football" jinsi unavyojulikana unawekwa karibu naye wakati wote, una namba ambazo atatumia kujitambulisha wakati anaamrisha makamannda kufanya shambulizi la nuklia.
Kisha inafuatia shughuli ya watu kadhaa na teknolojia ngumu ya kuchukua hatua ya kufanya shambulizi la nuklia.
Msaidizi wa Obama akibeba mkoba wa silaha za nyukliaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNamba za siri za kufungulia silaha za nyuklia huwekwa kwenye mkoba ufahamikao kama "nuclear football"
Matamshi yake yamekuwa tofauti na ashasisitiza kwa kukosha utabiri ni muhimu wakati jeshi na mabomu nuklia hutumiwa
Ndoa za jinsia moja zitaendelea kutambuliwa?
Donald Trump amesema wakati wa mahojiano kuwa anapinga ndoa za jinsia moja licha ya yeye kudai kuwa ashahudhuria ndoa hiyo.
Waandamanaji wa kutetea ndoa za jinsia mojaHaki miliki ya pichaAFP
Amesema kuwa ni suala linalostahili kuamuliwa kwenye majimbo badala ya nchi nzima na alighadhabishwa na uamuzi wa mahakama mapema mwaka huu ambao ulihalalisha ndoa za jinsi moja kote nchini.
Lakini mapema mwaka huu alisema kuwa atawateua majaji wa mhakama ya juu kutupilia mbalia uamuzi huo.

Nini kitafanyika kwa kesi zake zilizo mahakamani?

Trump amehusishwa na kesi kadha ambazo ziko mahakani.
Kwa sasa Trump ana jumla ya kesi 75 zilizo mahakamani.
Kwa sababu kesi hizo zilipelekwa mahakamani kabla aingie ofisini, Trump atahitajika kufika mahakamani kuhudhuria kesi hizo.
Kama hatua ya kujikinga, aliamua kulipa kumaliza baadhi ya kesi hizo siku chache baada yake kuthibitishwa kuwa mshindi wa urais Marekani.

Mimi ni Mwislamu, bado nitaruhusiwa kuenda likizo nchini Marekani?
Baada ya ufyatuaji mkubwa wa risasi mwaka uliopita mjini San Bernardino ambapo watu 14 waliuawa, bwana Trump alitaka waislamu wote wazuiwe kuingia nchini Marekani.
Matamshi hayo yalikosolewa kote duniani na hata kutoka kwa mgombea mwenza Mike pence ambaye aliyataja kuwa yanayokiuka katiba.
Miezi kadha iliyopita Trump ameonekana kuachana na mipango hiyo.

Trump anaweza kubatilisha mikataba kuhusu mabadiliko ya tabia nchi?
Bw Trump haamini binadamu amechangia mabadiliko ya tabia nchi na anataka Marekani ijitoe Mkataba wa Paris.
AntarcticHaki miliki ya pichaPA
Hata hivyo Mkataba wa Paris tayari umetiwa saini na sasa ni sehemu ya sheria za kimataifa. Ingawa Trump anaweza kupata wanasiasa wa kumuunga mkono kuondoa Marekani kutoka kwa mkataba huo, shughuli ya kujiondoa rasmi inaweza kuchukua hadi miaka minne.

Trump atadhoofisha Nato na kuweka hatarini washirika wa Marekani?
Bw Trump amekuwa akisema washirika wa Marekani wanafaa kulipia ulinzi wanaopata kutoka kwa Marekani. Anataka kutathmini upya mchango wa Marekani katika shirika la kujihami la nchi za Magharibi, Nato.
Julai alisema iwapo nchi za Nato zitashambuliwa na Urusi, zinafaa kutarajia Marekani izisaidie iwapo zimekuwa zikitimiza masharti pekee.
Baada yake kushinda, baadhi ya viongozi wa Ulaya wamemtaka kufafanua. Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg amemkumbusha kwamba mkataba huo hauna masharti.
Bado haijabainika iwapo ataweza kufikia maelewano na wanachama wa Nato.

Trump atashambulia Korea Kaskazini?
Mei, alisema anaweza kuketi na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kujaribu kuizuia Pyongyang isiendelee na mpango wake wa nyuklia, jambo ambalo ni tofauti na msimmao wa Marekani.
Alisema: "Ninaweza kuzungumza naye, sina tatizo kuzungumza naye."
Korea Kaskazini imemtaja kama "mwanasiasa mwenye busara" na wa "kuona mbali".
Korea Kaskazini imesema wazi kwamba haiko tayari kuacha kustawisha silaha za nyuklia.
Bw Trump amesema anaweza kuruhusu Japan na Korea Kusini anzo zistawishe silaha za nyuklia kama kinga dhidi ya Korea Kaskazini na Uchina.

Wamarekani watahamia sana Canada?
Baada ya ushindi wa Trumo, mtandao wa uhamiaji wa Canada ulipata hitilafu, watu wengi walipoutembelea labda kutaka kujua utaratibu wa kuhamia Marekani.
Ingawa ni rahisi Wamarekani kupata visa ya kwenda Canada, kuna masharti mengi iwapo mtu anataka kuhamia kabisa nchini humo.

Trump anaweza kuzuiwa kuzuru Uingereza?
Mwaka 2015 kulianzishwa ombi la "Block Donald J Trump from UK entry" (Mzuie Donald J Trump kuingia Marekani) kwa sababu ya matamshi ya uchochezi, baada yake kusema Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Ombi hilo lilipata saini zaidi ya nusu milioni na likajadiliwa bungeni Uingereza Januari 2016.
Ingawa ulijadiliwa, hakukupigwa kura yoyote hivyo hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa.

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*