Mvumbuzi wa Ghana azindua magari yake ya kifahari



Gari la Katanka lilivumbuliwa na Kwadwo SarfoImage copyrightMYJOYONLINE.COM
Image captionGari la Katanka lilivumbuliwa na Kwadwo Sarfo
Mvumbuzi mmoja wa Ghana ameonyesha kile anachotaja kuwa uvumbuzi wake wa hivi karibuni unaoshirikisha magari katika maonyesho ya Kiteknolojia katika mji mkuu wa Accra.
Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya Katanka na mbaye pia ni kiongozi wa dini alionyesha gari alilotengeza aina ya V8, pikipiki za magurudumu matatu, mashine za roboti za kuchomelea vyuma miongoni mwa vinginevyo.
Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya Katanka na rais wa Ghana kulia Nana Akofu AdoImage copyrightMYJOYONLINE.COM
Image captionKwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya Katanka na rais wa Ghana kulia Nana Akofu Ado
Rais Nana Akofu-Addo, ambaye alihudhuria maonyesho hayo amesema serikali yake itaangazia kuhusu elimu ya sayansi na teknolojia ili kuimarisha maendeleo ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Joy News.
Magari ya kantankaImage copyrightMYJOYONLINE.COM
Image captionMagari ya kantanka
Bw Sarfo ambaye ni babake mbunge mmoja amesema kuwa uvumbuzi wake unaonyesha uwezo mkubwa wa mtu mweusi katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi.
Alitengeza gari lake la kwanza mwaka 1998 na tangu wakati huo chapa yake ya Kantanka imetoa magari kadhaa ikiwemo magari yenye magurudumu manne na SUV.
Gari la magurudumu matatu lililotengezwaImage copyrightMYJOYONLINE.COM
Image captionGari la magurudumu matatu lililotengezwa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.