Ndege zisizo na marubani kubeba abiria 'kufikia 2020'



Cormorant UAVImage copyrightURBAN AERONAUTICS
Image captionNdege hiyo huenda itatekeleza mchango muhimu wakati wa mikasa, hasa mashambulio ya kigaidi
Kampuni moja ya Israel imesema ndege isiyokuwa na rubani, ambayo ilikamilisha safari yake ya kwanza kabisa ikipaa juu ya maeneo tambarare mwezi Novemba, huenda ikaanza kutumika rasmi kufikia 2020.
Ndege hiyo imeundwa na kufanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka 15, lengo likiwa kutumika katika juhudi za uokoaji au shughuli za kijeshi.
Ndege hiyo ambayo inafahamika kwa sasa kama Cormorant iligharimu $14m (£11m) na inaweza kubeba mizigo ya uzani wa kilo 500 (1,100lb) na kwenda kwa kasi ya kilomita 185 kwa saa (115mph).
Kampuni ya Urban Aeronautics imesema ndege hiyo ina rafadha (mapanga yanayozunguka kwa kasi ili kuendesha chombo) zilizo ndani na hilo linaifanya kuwa salama zaidi kushinda helikopta.
Kandi na kuweza kupaa juu na kutua bila kuhitajika kusonga mbele au nyuma, inaweza kupaa kupitia kati ya majumba na hata kupitia chini ya nyaya za umeme.
Cormorant UAVImage copyrightURBAN AERONAUTICS
Image captionNdege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza Novemba
"Hili linafungua njia ya kustawisha Cormorant kutoka kwa hatua ya majiribio hadi uzalishaji kamili karibuni na hatimaye kuanza kutumiwa kibiashara kwa teknolojia hii - kwa shughuli mbalimbali," alisema afisa mkuu mtendaji wa Urban Aeronautics Rafi Yoeli.
Ndege zisizo za rubani zimeanza kupata umaarufu katika kutumiwa kibiashara.
Amazon majuzi walitangaza kuanzishwa kwa huduma ya Prime Air, ambapo ndege zisizo na rubani zinatumiwa kusafirisha bidhaa kwa wateja.
Mwezi Juni, ndege nyingine isiyo na rubani ambayo iliungwa na kampuni ya Ehang kutoka China ilipewa idhini ya kufanyiwa majaribio jimbo la Nevada, Marekani.
NdegeImage copyrightTHINKSTOCK
Image captionNdege zisizo na marubani zinatumiwa na Amazon kusafirisha bidhaa kwa wateja
Mtaalamu wa ndege zisizo na marubani Ravi Vaidyanathan anasema mafanikio ya safari ya majaribio ya ndege hiyo ya Israel ni ufanisi mkubwa na kwamba ni uamuzi wa busara kwanza kuitumia kwa juhudi za uokoaji na shughuli za kijeshi.
Lakini ingawa huenda muda mfupi baadaye zikatumiwa kwa safari za kiraia - na kusaidia kufika hasa maeneo yasiyo na miundo mbinu au yenye misongamano ya magari - bado ni mapema kujua hilo litatekelezwa kikamilifu linu.
"Kuna changamoto nyingi za kihesheria, mfano kuhusu ni wapi unaruhusiwa kupaa? Ni wapi unaweza kutua? Unaruhusiwa kupaa juu hadi wapi?" alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*