NJAA YAPIGA HODI KILOLO ,DC APIGA MARUFUKU UTENGENEZAJI POMBE KWA KUTUMIA NAFAKA


Mwenyekiti  wa  kitongoji  cha  Kimala  wilaya ya  Kilolo  Barnabas Nyamoga  akionyesha shamba lake  ambalo mahindi yamedumaa kwa  kuchanua na kuanza  kukauka kabla ya  kuzaa
Shamba  la mahindi kijiji  cha Idunda Kata ya  Kimala  likiwa limekauka  kutoka  na  jua huku  mahindi  yakiwa hayajazaa
Mwenyekiti  wa Halmashauri ya  Kilolo Valence Kihwaga akionyesha  mashamba  ya  wananchi  wa Kimala  ambayo mahindi yameanza kunyauka  bila kuzaa  kutokana na kukosekana kwa  mvua ya  kutosha
mashamba ya  mahindi  yakiwa  yameanza  kukaaka  Kimala Kilolo
 
Na MatukiodaimaBlog 
KUNA  kila  dalili  ya  wananchi  wa wilaya ya  Kilolo kukumbwa na  njaa ya  kutisha  kutokana na baadhi yao  wakazi  wa kata ya  Kimala kuanza kujihami mapema   kula majimbi  baada ya mashamba  yao ya  mahindi  kukauka  kutokana na uhaba  wa  mvua ,huku  serikali ya  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  ikipiga marufuku utengenezaji  wa pombe ya mahindi  maarufu kama komoni.

Wakielezea  hali   hiyo ya  ukosefu  wa mvua  katika kata  hiyo  mwenyekiti  wa  kitongoji  cha  Kimala  Barnabas Nyamoga  jana  alisema kuwa  kwa kawaida kila  mwaka  mwezi  wa kwanza  wananchi wa  maeneo hayo ya  milimani huwa wanakula mahindi mabichi na mwezi  wa  tatu  huwa  wanavuna ila kwa  mwaka huu hali ni tofauti kwani bado  hawajaanza  kula mahindi mabichi  kutokana na  mvua  kushindwa kunyesha na badla yake  mahindi waliyopanda yameanza kukaua kabla ya kuzaa .

Nyamoga  alisema kuwa  wananchi  wamejitahidi  kulima hekari za  kutosha  wengi  wao  wamepanda kwa wakati ila mazao yao  yameishia  kukauka hali  inayowatia wasiwasi    na kupelekea  baadhi yao kuanza  kujihamia kwa  kula majimbi kwa  kuhofu  njaa.

"Huku  kwetu  kwa kawaida mwezi  huu wa  kwanza  huwa tunakula  mahindi mabichi  na ukifika mwezi wa  pili  mwishoni ama  wa  tatu mwanzoni ni  wakati wa  kuvuna ila  kwa hali hii hatujui  tutafanyaje maana  mahindi yamekauka  baada ya  kuchanua na mengine  hataka kabla ya  kuchanua "

Tayari  mbunge  wa   jimbo la  Kilolo Veanance Mwamoto amewataka watendaji  wa kata zote za  Kilolo  kutoa taarifa  mapema juu ya wananchi wanaokabiliwa na njaa ili  kuweza  kusaidiwa kwani  alisema serikali haitapenda  kuona mwananchi  wake anakufa kwa njaa.

Mwamoto amekuwa akitoa kauli  hiyo kwa  nyakati tofauti  wakati wa  ziara  zake zinazoendelea  jimboni humo kwa ajili ya kukagua  na kushiriki  shughuli za  kimaendeleo wilayani  humo ,kuwa ni  vema watendaji  wa kata  na  vijiji  kutoa  taarifa mapema ya  wazee ,wajane na  wananchi  wanaosumbuliwa na ukosefu  wa chakula   ili wasife  njaa.

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  akizungumza katika mazishi ya  aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo    na diwani wa kata ya  Kimala Mejus Mgeveke  jana  katika kijiji cha Idunda alisema kuwa hali  ya hewa  si nzuri na kuna uwezekano   mkubwa wa  wananchi  kukumbwa na tatizo la njaa  hivyo  ili  kujihami  na hali hiyo ni vema kuachana na matumizi mabaya ya  mahindi .

Mkuu   huyo alitaka  watendaji wa vijiji na kata  kuwachukulia hatua  sitahiki zisizo vunja haki za binadamu  wale  wote  watakaobainika kutumia  vibaya  mahindi   kwa kutengeneza pombe za  kienyeji .

Kwani  alisema  iwapo  wananchi  wataendelea  kutumia vibaya  mahindi  kwa  kutengeneza  pombe badla ya  kuhifadhi kwa ajili ya chakula   upo uwezekano  wa kukosa  chakula  kutokana na mvua  kushindwa  kunyesha   vizuri  hali  inayotokana na mabadiliko ya  tabia nchi  .

"Sitapenda  kuona mtu  yeyote katika wilaya  ya Kilolo akitumia  vibaya  mahindi kwa  kupika  pombe za  kienyeji  natambua wazi  kuwa baadhi  hutegemea  kuendesha maisha yao kwa biashara  za pombe na baadhi hutegemea  kutumia pombe kama sehemu ya burudani kwao  ila nawaombeni  sana hali ya  mvua  si nzuri  ni  vema kusitisha  matumizi ya mahindi kwa  kutengeneza  pombe na badala yake yatumike kwa chakula pekee"

Aidha  mkuu   huyo  wa  wilaya aliwaomba  wananchi  wenye  akiba ya kutosha ya  chakula  kuwauzia  wasio  na akiba kwa bei ndogo ya kusaidiana  badala ya  kuwauzia kwa bei kubwa .

" Nawaombeni  sana wananchi  wangu  tupendane wapo ambao  wana akiba ya  chakula  cha kutosha basi msaidianeni kwa  kuwauzia wengine kwa bei  ya  kawaida na wenye  chakula msichezee chakula "

Hata  hivyo  alisema  pamoja na  mvua  kutonyesha kwa  uhakika bado  wananchi  wanapaswa  kujiandaa  kulima mazao yanayohimili  ukame na mbegu  nyepesi  ili mvua  zitakapoanza kunyesha mazao hayo yaweze  kuendana na mvua   hizo .

Uchunguzi wa mtandaohuu wa matukiodaimaBlog unaonyesha  katika  maeneo  mbali  mbali ya wilaya ya  Kilolo yakiwemo ya  milimani  ambako kila mwaka mwezi kama  huu  huwa wamepanda na  kuanza  kupalilia ama  kula mahindi mabichi hali  hiyo ni tofauti kwa  mwaka huu sehemu kubwa  wakulima hawajapanda  wengine  hawajalima  huku kata kama  za  Kimala  ambazo huwa wanaanza  kula mahindi  baadhi  wamepanda na mazao yao yamekauka kabla ya kuchanua   huku  baadhi ya maeneo kama Masege, Pomerini , Kidabaga  Mbigili na Uwambingeto wengi  wao  hawajapanda
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA