4x4

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA KIJIWE CHA RAFIKI YAKE SHOE SHINER CHATO

 Rais John Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia viatu kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika Stendi ya zamani ya Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa aking’arishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha nyuma.

 . Rais John Magufuli akifurahia pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita leo. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza hadi la Saba. Rais amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwa sababu yeye pia alisoma shuleni hapo. (PICHA NA IKULU)


Post a Comment