Riyad Mahrez mchezaji bora Afrika



Mahrez ameisaidia Leicester City kutwaa ubingwa msimu uliopita
Image captionMahrez ameisaidia Leicester City kutwaa ubingwa msimu uliopita
Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Mahrez mwenye miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.
Mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo pia.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Mahrez ameshinda pia tuzo ya mchezaji bora wa BBC Afrika
Image captionMahrez ameshinda pia tuzo ya mchezaji bora wa BBC Afrika
Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani.
Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA