4x4

SPIKA NDUGAI ALIPOHUDHURIA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis mara baada ya kumalikiza kwa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud mara baada ya kuwasili katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (mwenye suti nyeusi katika) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka korea ya kusini mara baada ya maongezi mafupi yaliyoambatana na chakula cha mchana katika hotel ya serena, Baada ya kutoka katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Post a Comment