TAARIFA KWA UMMA UTOAJI RUZUKU AWAMU YA TATU KWA WACHIMBAJI MADINI WADOGO, 16 JANUARI 2017, MPANDA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI


TAARIFA KWA UMMA
UTOAJI RUZUKU AWAMU YA TATU KWA WACHIMBAJI MADINI WADOGO, 16 JANUARI 2017, MPANDA.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) itatoa Ruzuku ya  jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji Madini Wadogo 59 ambapo kiwango cha juu cha Ruzuku kwa Kikundi/Mtu binafsi kikiwa ni  Shilingi Milioni 210.
Hafla ya utoaji wa Ruzuku hiyo itafanyika siku ya Jumatatu , tarehe 16  Januari 2017, Mjini Mpanda mkoani Katavi, Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim  M. Majaliwa (Mb.).
Fedha za Ruzuku kwa kila Mnufaika, zitatumika kununua vifaa vya kuchimbia au kuchenjulia madini ambapo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, wanufaika hao watapata mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya ruzuku yatakayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 15 Januari, 2017 Mjini Mpanda.
Miradi 59 itakayopata ruzuku hiyo, ndiyo iliyoshinda kati ya miradi 592 ya uchimbaji madini mdogo iliyokuwa kwenye ushindani.. Waombaji wengine ambao maombi yao hayakushinda watajulishwa kwa Barua.
Wizara ya Nishati na Madini ilianza mchujo wa kuwapata Washindi tangu Mwezi Julai 2016, kwa kuwashirikisha , Viongozi wa Wachimbaji Madini Wadogo wa mikoani (REMA’s),Viongozi wa Kitaifa  (FEMATA) pamoja na Viongozi wa Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA).
Majina ya wanufaika wa Ruzuku awamu ya tatu  pia yanapatikana kwenye Tovuti ya Wizara:www.mem.go.tz pamoja na Ofisi Za Madini Za Kanda.
Imetolewa na,
                                        

Prof. Justin W. Ntalikwa

KATIBU MKUU

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*