TAASISI YA MOYO YA JAKAYA YAPONGEZWA



             
   NA ANGELLA MSANGI,DAR ES SALAAAM

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam  wamepogeza huduma mbali mbali za matibabu  zinazotolewa kwenye Taasisi ya moyo ya jakaya kikwete iliyopo kwenye hospitali ya Taifa ya  Muhimbili ambapo wamesema kuwa kwa sasa matibabu ya moyo yamepata ufumbuzi tofauti na miaka mingine ilivyokuwa hapa nchini.

Wakizungumza wakiwa hospitalini hapo baadhi ya wananchi hao waliokuwa katika nyuso za furaha baada ya kupata huduma nzuri wamesema kwamba hospitali hiyo inafaa kuwa ya kuigwa kutokana na namna ya huduma zinavtolewa kuania madakitari mpaka wauguzi na watoa huduma wa kawaida.

Reuben Mtaita  (79) mkazi wa Kongwe nje kidogo ya jiji la Dar es salaam amesema tangu ameanza kutibiwa katika hospitali hiyo amwezakupata nafuu kwa matatizo ya moyo yanayomsumbua huku akisema kwamba huduma ziko katika viwango na hujutii kupata matibabu katika hospitali hiyo.

“Yaani hii hospitali inatoa huduma bora kabisa , hata namna madakitari wanavyokuhudumia inatia moyo na kwamba wako karibu na wagonjwa kuhakikisha unaapata matibabu sahihi”alisema Mtaita 

Kwa upande wake mkazi wa Temeke Khadija Omary (30) amesema anafuraha huduma za hospitali hiyo na kwamba tangu aanze utibiwa ameona unafuu mkubwa na kwamba hali yake inazidi kuimiraika.

“Huduma zipo kwenye ubora na wagonjwa tuna hudumiwa bila ubaguzi hili jambo limenifurahisha kabisa”alisema Khadija .

Baadhi ya madakitari, Bashir Nyangasa  na George  Longopa  wamesema kwamba wanajitahidi kwa uwezo wao kuhakiksha wagonjwa wanapata matibabu ya uhakika na yenye viwango vya juu ili kuhakikisha wagonjwa wa moyo wanakuwa salama .

“Tunajitahidi kwa uwezo wetu kuweza kuwahudumia wagonjwa wote wanaofika katika taasisi yetu katika kiwango cha hali ya juu na kama uliyoona mwenyewe wagonjwa wanaridhika na matibabu waayopata” alisema dokta Nyangasa 
akiongea na mwadishi

Naye mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya Moyo ya Jakaya Kikwete Professa Mohamed Jahabi amesema kwamba ,katika hospitali hiyo wanaendelea kutoa huduma zilizo bora na kuwashauri wananchi nchini kujiuga na huduma za bima afya ili kuweza kumudu gharama za ugonjwa wa moyo katika matibabu na vipimo
vyake.

“Mwananchi akiwa kwenye mpango wa bima ya afya ni rahisi sana ana unafuu katika kutibwa kwani ni gharama kubwa , lakini mtu anapokuwa amejiunga katika mfuko wa bima ya taifa unaweza kugharimia “ alisema dokta Jahabi .

Amesema kwa sasa hospitai hiyo iamdelea na maboresho mbali mbali hasa katikaeneo la huduma kwa wateja ambapo amesema wafanyakazi waliopo katika idara hiyo wanapataiwa mafunzo mbali mbali ya kuweza kuhudumia wagnjwa wanaokuja katuka taasisi hhiyo.

Kwa mujibu wa dakta Jahabi mpaka sasa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 mwaka jana iliweza kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa wenye jumla ya 973 ambapo ameongeza kuwa hospitali hiyo imepunguza kwa asilimia 80 kwa wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa na badala yake hutibiwa hapa nchini katka hospitali hiyo kutokana na wataalamu waliopo .

Hata hivyo amesema mbali na wagonjwa wa hapanchin kutibiwa katika hosptali hiyo pia wagonjwa kutoka nchini za comoro,burundi congo na uganda wamekuwa
wakitibiwa katika taasisi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.