VIDEO FUPI: Maamuzi mapya ya Waziri Mwigulu kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji


Wakati mwaka 2016 ulipokaribia mwishoni kulitokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji huko wiliyani Kilosa mkoani Morogoro, sababu ikatajwa kuwa wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kitu kilichosababisha wengi wao kukatwa mapanga na kuchomwa mikuki.
Leo January 3, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefika katika kijiji cha Tindiga kilichopo wilaya ya Mikumi zilipotokea vurugu zilizopelekea mkulima mmoja kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa Kilosa kabla ya kutoa maamuzi. 
Waziri Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio lolote la watu kuuana kwa mapanga, mikuki, sime  na silaha zozote za jadi zinazotumiwa hasa na wakulima na wafugaji, serikali itafuta utaratibu wa kubeba silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama watuhumiwa wengine.
Kinginie alichoagiza Waziri Mwigulu ni wakuliam na wafugaji kwa pamoja kuwakamata watu wote watakaohusika na kuanzisha vurugu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kabla jeshi la polisi halijafanya maamuzi yake.  

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*