WANAFUNZI WA TUDARCo WATOA MSAADA HOSPTALI YA PALESTINA


 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Tumaini mwaka wa tatu wakiwa katika picha ya pamoja chuoni hapo. 

 Afisa Mhuguzi wa Hospitali ya Sinza Palestina, Aliho Ngerageza (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa wanafunzi wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar  es Salaam (Tudarco), kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa hospitalini hapo anaekabidhi ni Enock Bwigane  na katikati ni Mhadhiri wa somo hilo chuoni hapo, Mary Kafyome 

 Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome akizungumza na vyombo vya habari.
 Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome akitoa msaada kwa mgonjwa aliyelazwa hosptalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 Wanaochangia damu  wa kwanza kushoto ni Marietha Tairo na Ole Kimosa,aliyesimama ni nesi akisaidia kufanikisha zoezi hilo.


 Mhadhiri wa somo la Public Relations chuoni hapo, Mary Kafyome wa kushoto akiwa na Sara wakiendelea na kufanya usafi.

 Baadhi wa wanafunzi wakifanya usafi katika Hosptali ya Palestina.

(Picha na Evance Ng'ingo)

Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
Wanafunzi wa mwaka wa tatu  wanaosoma Shahada ya Mawasiliano ya Umma, katika Chuo Kikuu cha Tumaini (TUDARCo), kwa udhamini wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), jijini Dar es Salaam.
wametembelea hospitali ya Sinza (Palestina) na kutoa msaada wa vitu mbali mbali,pamoja na kuchangia damu ili kusaidia kuokoa wajawazito na majeruhi wanaofika hosptali hapo kupatiwa matibabu na kujifungua.
Mbali na msaada huo wa vifaa vya watoto vikiwamo maji, juisi, nepi na vifaa vya usafi, wanafunzi hao pia walijitolea kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusaidia na kujenga mahusiano mema na jamii inayowazunguka katika somo la Mahusiano ya Umma (Public Relations).
Muuguzi Gerangeza alisema hospitali yake imefurahi kupokea msaada huo hasa damu kwani hospitali ina upungufu wa damu kutokana na kupokea wagonjwa wengi wenye uhitaji wa damu.
“Mahitaji ya damu ni makubwa kwa siku tunatumia uniti sita hadi 10, kwani kwa siku tunapokea wajawazito 30 hadi 35 ambao wanahitaji damu, wakati mwingine huwa tunaazima Hospitali ya Amana au Mwananyamala.
“Kwa hiyo tunawashukuru sana kwani damu haipatikani dukani isipokua kwa wasamaria kama ninyi naomba na vyuo vingine na taasisi waige mfano wenu,” alisema Gerangeza.
Mwalimu wa somo la Mahusiano ya Umma, aliyeambatana na wanafunzi hao, Mary Kafyome alisema licha ya zoezi hilo kuwa ni sehemu ya somo lakini pia ni kuunga mkono juhudi za serikali za kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka.
“Rais anahamasisha usafi tukaona ni vyema nasi mbali na kutoa msaada tumuunge mkono. Lakini pia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kwa sababu ya kukosa damu.
“Pia naomba nitoe wito kwa vyuo vikuu, tuhakikishe tunawajenga wanafunzi wetu kwa vitendo si kufundisha darasani pekee, naamini watakuwa mabalozi wazuri wa vyuo vyetu katika taasisi watakazoenda kufanyia kazi katika kusaidia jamii hata kwa faida ndogo waliyoipata,” alisema Kafyome.
Baadhi ya wanafunzi walisema wamefurahia zoezi hilo kwani linawajenga kuwa maofisa uhusiano bora katika taasisi na kampuni watakazofanyia kazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA